Na Pendo Mkonyi, Arusha.
Shule ya sekondari Mwandeti ya mkoani arusha imeendelea kuwa kinara kutokana na matokeo yake mazuri kufuatia mwaka huu wa 2023 tena katika matokeo ya kidato Cha 6 kufaulisha Kwa daraja la kwanza watahiniwa wote 77.
Akizungumza mara baada ya kutangazwa Kwa matokeo ya kidato Cha 6 nchini mkuu wa shule ya sekondari Mwandeti John Silvano Masawe amesema kuwa wanafunzi wote 77 waliofanya mitihani Yao ya kidato Cha 6 wamefaulu Kwa kiwango Cha juu na hawezi kulinganishwa na shule ya sekondari Ilboru na kisimiri
Pichani: ni mkuu wa shule ya sekondari Mwandeti John Silvano Masawe.
Masawe amesema kuwa shule ya sekondari mwandet imekuwa ikifuliliza Kwa kufanya vizuri hatua Kwa hatua Kwa lengo la kukamilisha maono na mtazamo wa kutoa elimu Bora wilaya ya Arusha na mkoa wa Arusha Kwa ujumla,na shule hiyo siyo kama iliboru sekondari Wala kisimiri kwani wanafunzi wanoteuliwa hapo kujiunga na kidato Cha 5 ni wale wa daraja 3 la mwisho tofauti na shule zingine
Alisema shule ya sekondari Mwandeti ilianza kutoa elimu katika mazingira magumu sana kwani shule hiyo ilianzishwa mnamo tarehe 05/04/2004 ikiwa na jumla ya wanafunzi 28 wavulana 12 na wasichana 16 pamoja na waalimu 2 tu ila kwasasa ina wanafunzi takribani 1726 wakiwemo wavulana 655 na wasichana 980 katika Yao 78.
Masawe amesema kuwa historia ya shule hiyo imeendelea kubadilika kwani hivi sasa shule ina majengo mazuri na mazingira Bora na rafiki ya kujisomea ikiwepo usafiri wa kuwawezesha waalimu kufika shuleni Kwa wakati.
Wanafunzi wa shule hiyo hawana Muda wa kupoteza kwani hujisomea ipasavyo hata katika masomo yao ya ziada nyakati za jioni Huku wakisaidiwa na waalimu wao Kila wakati wawapo hostel
Akitaja matokeo ya kidato Cha sita tangu shule ifunguliwe 2018 mtihani wa kidato Cha 6 walukuwa watahiniwa 29 ambapo daraja la kwanza walikuwa wanafunzi 26 na daraja la pili wanafunzi 3
Masawe amesema kuwa shule ya sekondari Mwandeti wakati huo ilishika nafasi 2 kimkoa na ya 4 kitaifa mwaka 2019 na mwaka 2020 walikuwa na watahiniwa 43 na waliopata daraja la kwanza walikuwa wanafunzi 37 na daraja la pili wanafunzi 6 mwaka 2021walikuwa watahiniwa53 daraja la kwanza walikuwa wanafunzi 51 na daraja la pili wanafunzi 2,mwaka 2022 walikuwa watahiniwa54 ambapo daraja la kwanza lilikuwa ni wanafunzi 45 na daraja la pili wanafunzi 9 na mwaka 2023 walikuwa watahiniwa 77 na wote walifaulu Kwa daraja la kwanza hakuna daraja la pili au la tatu.
Alisema kuwa shule hiyo haifananani na yeyote hapa mkoani arusha “naposema haifananani na shule ya sekondari kisimiri na iliboru sitanii namaanisha kwani sisi Mwandeti tunaletewa wanafunzi wa daraja la tatu la mwisho ambapo hawako vizuri kimasomo tunaanza kuwajenga ukilinganisha na wanafunzi wa kisimiri na iliboru wanaopewa wanafunzi wenye daraja la kwanza nukta saba”
Mwaka huu 2023 watahiniwa wote wamefaulu ambapo wakijitazama kimkoa wapo nafasi ya pili au kwanza na kitaifa wanaweza kuwa nafasi ya 8 kutoka 32 hivyo wanamshukuru Mungu na wamejipanga matokeo kuwa Bora zaidi.
Baraza la mtihani ni vema likarejesha mashindano ya kitaaluma Kwa kupanga ngazi kuanzia nafasi ya kwanza mpaka ya mwisho ili kuleta zile juhudi kwani shule nyingi Sasa ni kama zimepata kichaka Cha kujificha kwasababu ya Kila mmoja kusema amefanya vizuri tofauti na hapo zamani hata wazazi walikuwa wakijua shule ipi inaongoza na ipi ipo nyuma. Na nashauri zawadi ziwepo Kwa shule zinazofanya vizuri na vinyago Kwa zile zisizofanya vizuri zivalishwe.
Hata hivyo amempongeza daktari Samia suluhu Hassan na serikali ya jamhuri ya muungano ya Tanzania Kwa kuwajengea mabweni na Kwa kuboresha miundombinu ya shule ikiwemo kuwapa fedha za fidia ya ada na kuepusha usumbufu ambapo hali hiyo inawafanya wanafunzi kuondokana na vizuizi vya na kujikuta wakiwa bize na masomo.
Makamu mkuu wa shule ya sekondari mwandeti lekera Sakey amesema amefurahishwa na matokeo ya mwaka huu 2023 licha ya mwaka jana kutolewa kwenye 10 Bora hivyo wanajiona wanelekea kufika malengo Yao waliojiwekea, hapo lengo likiwa ni kushika nafasi ya kwanza kitaifa.
Mwalimu Prosper John Rushinga mwalimu wa kiswahili amekiri kufaulisha Kwa kiwango Cha A na B ambapo anaishukuru serikali Kwa kuwawezesha waalimu kuwalipa mishahara Kwa wakati pia shukrani zaidi ofisi ya mkoa na uongozi wa shule Kwa kushirikiana bega Kwa bega wakiwamo wazazi Kwa kutoa ushirikiano wa hali ya juu ndio maana matokeo hayo yamekuwa mazuri zaidi sana wanafunzi wao Kwa kuwa watii na wasikivu na kufanikiwa kwenda kujiunga na vyuo vikuu.
Dada mkuu wa shule hiyo Debora Emanuel amesema kuwa anampongeza mheshimiwa Rais Kwa kuwafutia ada kwani inawawezesha kujisomea Kwa bidii na pia anaishukuru shule hiyo kwani ni ndoto ya maisha yake,Rahel chalse anaishukuru shule hiyo Kwa kuwafunza vizuri.