Na Richard Mrusha mbeya
MAMLAKA ya Huduma ya Usafiri wa Anga imewahakikishia watanzania kwamba usafiri wa sekta ya Anga ni usafiri salama zaidi kulikos ekta nyingine.
Hayo yamesemwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushuari la watumiaji huduma za Usafiri wa Anga (TCAA-CCC) Innocent Kyara wakati akizungumza na waandishi wa habari siku ya kilele cha maoyesho ya wakulima katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
“Sekta ya usafiri wa anga ndiyo sekta salama zaidi kushinda sekta nyingine za usafirishariji kutokana na nguvu kubwa iliyowekwa katika kuhakikisha bidhaa ,wananchi wanasafiri salama.”amesema Kyara na kuongeza kuwa
“.Ajali za ndege hapa nchini zimekuwa zikitokea ni kwa nadra sana kutoka na juhudi za mamlaka katika kusimamia vile viwango” ametumia nafasi hiyo kuwaasa wananchi waendelee kutumia sekta hiyo kwani ni salama na uhakika wa usafirishaji.
Vile vile amesema sekta ya usafiri wa anga imekuwa na mchango mkubwa katika sekta ya kilimo na sekta nyingine.
Kyara amesema kuwa Wanashirikiana na Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu (TPHPA) ambao wanatumia ndege zisizo kuwa na rubani katika shughuli za kilimo na hivyo kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao.2
“Ndege hizo zinatumika katika kumwagilia dawa,zina uwezo wa kubeba lita 11 hadi lita 30 zote hizo ni jitihada kuhakikisha tija inaongzeka katika kilimo.”
Pia amesema ,serikali imeleta ndege ya mizigo huku akisema ni tegemeo lake kwamba wakulima wataitumia ndege hiyo kwa ajili ya kusafirisha mazao yao nje ya nchi .
“Wakulima watumie sekta ya usafiri wa Anga kusafirisha bidhaa zao lakini pia wazingatie viwango vya ubora katika bidhaa zao.”amesisitiza
Amesema Taasisi hiyo inanedelea kutoa elimu huku akisema katika maonyesho wametembelewa na watu zaidi ya 600 ambao anaamini nao watakwenda kuwa mabalozi wazuri kutokana na elimu waliyoipata na wao kwenda kuisambaza ili wengi zaidi waweze tuifahamu elimu ya anga na namna inavyoweza kuchochea sekta ya kilimo na sekta nyingine kwa ujumla.
Mwisho.