Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji(Mb.)
amekutana na kufanya mazungumzo kuhusu kuendeleza uhusiano wa kibiashara na China hususan katika uchakataji wa mazao ya kilimo na Balozi wa China nchini, Mhe. Chen Mingjian katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam Septemba 11, 2023. Tanzania inasafirisha mazao ya kilimo kama parachichi, kahawa, mahindi , ufuta na asali kwenda China.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo kuhusu kuendeleza ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji baina ya Tanzania na Uturuki hususan katika sekta ya kilimo katika mazao ya Chai, matunda na mazao ya misitu kama mbao pamoja ma upatikanaji wa soko la bodhaa za Tanzania na Balozi wa Uturuki nchini Mhe. Dkt. Mehmet Güllüoğlu Septemba 9, 2023 katika Ofisi ndogo za Wizara, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo kuhusu kuendeleza ushirikiano wa kibiashara baina ya Tanzania na Indonesia na Balozi wa Indonesia nchini Mhe. Tri Yogo Jatmiko Septemba 11, 2023 katika Ofisi ndogo za Wizara, jijini Dar es Salaam..
Waziri Kijaji amemhakikishia Balozi huyo kuwa Tanzania iko tayali kuendeleza ushirikiani baina ya nchi hizo na iko tayari kuwezesha miradi ya uwekezaji hususani katika sekta ya kilimo hasa katika uongezaji wa mnyororo wa thamani katika mazao ambayo nchi hiyo imepanga kuyaendeleza kama vile karafuu ili kuongeza ajira na kipato kwa wanzania.