Na Geofrey Stephen Arusha
Uongozi wa Club ya Aces ya jijini Arusha ambao ni waekezaji wa kitanzania wameadhimisha mwaka moja wa club hiyo kwa kurejesha faida kidogo kwa jamii kwa kufanya usafi wa mazingira pamoja na kugawa mapipa.ya kisasa ya kuifadhia takataka .
Akiongea katika maadhimisho hayo Mkuu wa Wilaya ya Arusha Felician Mtahengerwa amesema amefuraishwa kuona vijana wa kitanzania kufanya jambo kubwa kama hilo la kurejesha faida kwa jamii inayo izunguka kunufaika na uwekezaji mkubwa wa club hiyo ambapo ameomba uongozi huo kujikita pia katika kuchangia maendeleo ya sekta ya elimu Afya na miundo mbinu ya bara bara.
Felician Mtahengerwa amesema kupitia the Royal Towers ya Mh Rais Jiji la Arusha na viunga vyake imekua na mafanikio makubwa ususani wageni kutembelea maeno ya vivutio vya utalii pamoja na kulala katika Hotel nzuri jambo ambalo kumekua na mzunguko mkubwa wa kifedha kwa wananchi wa Arusha.
Kuwepo na uwekezaji mkubwa kama huu wageni baada ya kutembelea vivutio wanafika hapa kupata huduma muhimu ya vyakula pamoja na vinywa hii yote inaingizia pato serikali yetu ya wilaya mkoa na nchi kwa ujumla hili ni jambo la kujivunia katika mkoa wa kitalii.
Kwa upande wake Mwekezaji kijana wa kitanzania Arnold Balati mkurugenzi wa Aces amesema wanajivunia kwa uwekezaji katika nchi ya Tanzania jambo ambalo limewafanya kuajiri wafayakazi zaidi 80 ambao ni vijana wa kitanzania ikiwa ni sehemu moja wapo ya kupunguza ukosefu wa wa ajira nchini.
Balati amesema katika maadhimisho hayo ya mwaka moja wa club ya Aces wamechangia serikali ya mtaa vifaa vya kufanyia usafi mapipa ya taka taka na kwa sasa wamepanga kupeleka nguvu katika kusaidia sekta ya elimu kujenga madarasa na ujenzi wa matundu ya vyoo ktika kata Sekei .
Katika maadhimisho hayo ya mwaka moja wafanyakazi wa Aces walifanya usafi wa mazingira kuzunguka mtaa wa mahakama pamoja na mkuu wa wilaya Arusha kwa pamoja walifanya usafi wa mazingira na kuchoma taka na kutoa elimu ya mazingira .
Kwa upande wake mwenyekiti wa serikali ya mtaa Ahmed Chacha amepongeza zoezi la ufanyaji usafi ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Mh Rais la ufanyaji usafi kwa kila mwezi wenye lengo la kuweka mazingira ya watanzania safi .
Amesema kama serikali ya mtaa wanafuraha kubwa kuona wamepatiwa mapipa 10 ya kutunza mazingira hivyo kutaka uwekezaji huo kufikia jamii inayo zunguka kunufaika muda wote.
Picha za Matukio maadhimosho ya mwaka moja wa Aces Club Jijini Arusha .
Mwisho