Na Geofrey Stephen Arusha.
Wamiliki wa vyombo vya usafiri mkoani Arusha wamekutana kwa pamoja na Latra Tira na Jeshi la polisi na kufanya mazungumzo zaidi ya juu ya sheria za usafirishaji.
Akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kikao hicho afisa wa latra mkoa wa Arusha Joseph Michael amesema kuwa lengo la mazungumzo hayo ni kupeana elimu na ufafanuzi wa sheria kanuni na taratibu za usalama barabarani.
Amesema kuwa mara baada ya elimu hiyo mkoa wa Arusha unategemewa kuwepo Kwa ufanisa mkubwa na mabadiliko makubwa katika sekta ya usafirishaji.
Afisa Latra huyo amesema kuwa kuanzia tarehe 1/10 Hadi tarehe 14/10 madereva wote Kwa mujibu wa sheria no 5 kifungu Cha kwanza E madereva wanapaswa kusajiliwa na kuthibitishwa na Latra Kwa madereva wenye Madaraja ya leseni C C1,C2 C3 na E
Wamiliki wote wamekumbushwa kutuma maombi mapema kabla ya leseni zao kuisha kwenye mfumo wa Rim ili waweze kupata leseni ambapo mtu binafsi anapaswa kuwa vielelezo vifuatavyo ikiwemo namba ya Nida,kopi ya kadi ya gari,kopi ya hati ya bima,na ukaguzi wa polisi.
Madereva ili waweze kusajiliwa wanapaswa kuwa na Nida, cheti Cha mafunzo na leseni ambapo ametoa wito Kwa wamiliki wote kuhakikisha wamefuata utaratibu huo.
Mrakibu mwandamizi wa jeshi la polisi Bi Sauda Mohamed mkoani arusha amewashukuru wadau waliotoa elimu pamoja na wamiliki waliohududhiria katika mafunzo hayo ambapo amewataka madereva kutoa ushirikiano pindi wanapokutana na changamoto mbalimbali kwani amesema kuwa
ofisi yake ipo wazi na wasaidizi wapo ili kutatua changamoto wanazokabiliana nazo pindi wapo barabarani.
Mwenyekiti wa kamati iliyoundwa na wamiliki wa daladala Gerald Muniss amesema kuwa lengo la kuundwa kamati hiyo ni kushirikiana na taasis za serikali lengo likiwa ni kuangalia kuona namna gani kufanya usafiri huo kuwa wa kisasa zaidi
Hata hivyo wamiliki wengi walionekana kukosa uelewa kuhusu mambo ya usafirishaji kutoka latra,bima pamoja na Tra ndio maana semina hiyo imeandaliwa ambapo semina hiyo imeonekana kuwafungua.
Afisa Bima Caroline Modest kutoka Mamlaka ya usimamizi wa bima Tanzania TIRA Kanda ya kaskazini Amesema kuwa changamoto kubwa inayowakabili kukata Bima Kwa ada pungufu ambapo wakati mwingine hukuta kupitia chombo binafsi ili hali bima Ile inaenda kutumia kwenye gari la abiria.
Pichani ni Afisa Bima Kanda ya kaskazin Mamlaka ya usimamizi wa Bima Tira Bi Caroline Modest ku