Geofrey Stephen Hai.
Kamati ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo imekipongeza Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) Kampasi ya Kikuletwa ilioko Hai Mkoani Kilimanjaro kwa hatua nzuri ya ujenzi wa majengo matatu yaliyopo Wilaya ya Hai mkoa wa Kilimanjaro ambayo yanatarajiwa kuwa kituo cha umahiri katika nishati jadidifu.
Pongezi hizo zimetolewa wilayani humo na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo,Husna Sekiboko kwaniaba ya wabunge wa kamati hiyo walipotembelea kampasi hiyo ili kukagua maendeleo ya ujenzi wa majengo yanayotarajia kukamilika Januari 15,2024 .
Majengo hayo yanayogharimu dola za kimarekani 16,250,000.00 zilizotolewana Benki ya Dunia (WB) na yamegawanyika kwenye loti tatu ambazo ni mabweni ya wanafunzi,majengo ya kujifunza,kumbi ya mikutano ,maabara ,mgahawa na chumba cha umeme ikiwemo ujenzi wa mabwawa wa maji taka.
“Ninawapongeza ATC kwa kazi nzuri wanayoifanya kwa usimamizi, nawapongeza wakandarasi pia Wizara ya Elimu kutoa sapoti kwa vyuo vya ndani viweze kujitegemea na kushindana kimataifa”
Alisema Kampasi hiyo ikikamilika kujengewa itasaidia kutoa wataalamu ambao watasaidia kupunguza matumizi ya mkaa na kuni na kuleta nishati ambayo itakua rafiki kwa mazingira.
Naye Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Kilimanjaro, Ester Maleko na Mbunge wa Vyuo Vikuu,Dk,Thea Ntara waliomba wakandarasi wanajenga kampasi hiyo kuharakisha ujenzi huo utakaowakusanya wanafunzi kusoma na kuja na bunifu zenye tija zotakazotatua changamoto ya umeme nchini
Awali , Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia, Omar Kapinga alisema kampasi ya Kikuletwa inajengwa kwa ufadhili wa benki ya Dunia(WB) kupitia mradi wa Afrika Mashariki wa kujenga ujuzi na uingiliano wa kikanda (EASTRIP) ambao utaiboresha kampasi hiyo kuwa kituo cha umahiri katika nishati jadidifu.
Wakati huo huo, Mkuu wa chuo cha ATC,Dk,Musa Chacha ujenzi kituo Cha umahiri cha nishati jaddifu ulichaguliwa kufanyika Kikuletwa kutokana na uwepo wa vyanzo vya maji ya kuweza kuzalisha umeme lakini pia kinakabiliwa na upungufu wa fedha uliopelekea marekebisho ya michoro ya majengo na kupunguza WiGo wa kazi ya ujenzi na vifaa vya kujifunza na kufundishia.
Mwisho.