Na Mwandishi wa A24tv
Vijana wa familia za wakazi wa Vijiji vilivyoshamiri kwa kilimo cha bangi mkoani Arusha vya Kisimiri na Lesinoni wilayani Arumeru wametakiwa kuondokana na imani potofu ya kwamba bangi ndiyo kilimo kinachoweza kuwanyanyua kiuchumi kwa kuwapatia kipato cha kumudu mahitaji yao ya lazima yakiweo ada ya masomo.
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Nchi(DCEA) imelazimika kuendesha elimu juu ya madhara ya matumizi na biashara ya Dawa za Kulevya kwa wanafunzi 1,141 na walimu 45 pamoja na baadhi ya viongozi wa vijiji hivyo.
Elimu kwa kundi hilo la vijana imekuja baada ya Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya(DCEA) Kwa Kanda ya Kaskazini kufanya Operesheni katika kijiji cha kisimiri na Lesinoni na kubaini dhana hiyo imewaingia kwa watoto na Vijana wa maeneo hayo.
Kwa upande wao viongozi wa dini wamewataka wanafunzi hao kuzingatia elimu na kuachana na dawa za kulevya kama bangi.
Elimu hiyo imeongozwa na Sarah Ndaba ambaye ni Afisa ustawi wa Jamii wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya(DCEA) katika Kanda ya Kaskazini
Mwisho.