Na Mwandishi wa A24Tv Arusha
Kishindo cha wiki ya Asasi za Kiraia (AZAKI) yaanza kunguruma Jijini Arusha mapema leo ikiwa na wadau wa kutosha na kuanza kuamasisha jamii kupokea mabadiliko ya teknolojia na kutumia katika kunufaisha jamii .
Mkurugenzi wa Foundation for Civil Society Francis Kiwanga akiongea katika mkutano huo amesema kuna kila namna kukubali teknolojia katika kutambua changa moto zake na faida zake ambazo zimekua chachu ya maendeleo kwa watanzania na jamii kubwa Duniani
Mada nyingine ni ujumuishwaji na uwezashaji kidigitali, matumizi ya takwimu katika kuleta manufaa katika jamii, teknolojia na utetezi katika jamii, elimu na mafunzo ya kidigitali nchini Tanzania, teknolojia kwa maendeleo endelevu pamoja na kuimarisha usalama mtandaoni.
Mwakilishi wa shirika la Apple Inc kutoka nchini Marekani ambaye ni Mtanzania, Aboubakar Ally amesema mabadiliko ya kiteknolojia ya kidigital duniani kwa sasa imekua kwa kasi kubwa sana na matokeo mazuri hivyo jamii iwe tayari katika mabadiliko ya kidigital na kupenda kutumia
Mwisho .