Na Geofrey Stephen Arusha
Wadau Mbalimbali wanaotumia huduma zitokanazo na Teknolojia wameomba Taasisi za Fedha kurahisisha huduma hizo Kwa watu wenye ulemavu ikiwemo walemavu wa macho
Wakizungumza katika Mkutano wa Asasi za Kiraia (Azaki) unaofanyika mkaoni Arusha wadau hao wameomba kupatiwa mfumo shirikishi utakaowasaidia kwenye utumiaji wa Teknolojia katika maeneo Mbalimbali.
Renatusi Rupoli ambaye ni mlemavu wa macho kutoka Iringa amesema watu wasioona huwa wanatumia mitandao kwa njia ya sauti ambapo alihoji kwanini kusiwepo na Software kama hizo ambazo zinajumlishwa kwenye Mashine za Kutolea pesa (ATM) Benki Ili kupunguza usumbufu wakutafuta wasaidizi wakati wa kutumia huduma hizo.
Mtoa mada katika Mkutano huo Amali Baziadi kutoka Benki ya Stanbic amesema changamoto hiyo ameichukua na kwamba wataona namna gani yakulifanyia kazi ili kupata ufumbuzi.
“Ninaimani kuwa siyo tu Stanbic pekee ambao hatuna huduma hii lakini naichukua kama changamoto na tuone namna gani tunaifanyia kazi ili kuwawezesha wateja wetu kupata huduma rafiki kwao”amesema Baziadi.
Washiriki wa Mkutano huo wameendelea kushauri kuwepo kwa huduma rafiki Kwa wazee na wananchi waishio Vijijini namna ambavyo wanaweza kufungua akaunti za Benki kwa kutumia mitandao badala ya kufuata huduma hizo kwa mawakala wa Benki ambao mara nyingi hupatikana mijini.
Mkutano huo ulianza mapema wiki hii ambapo ASASI za kiraia zimeangazia zaidi matumizi sahihi ya teknolojia Kwa Jamii ambapo washiriki wamkutano huo wametikea katika mashirika Mbalimbali yasiyo ya kiserikali, na wadau Mbalimbali wa Teknolojia.
Mwishooo.