Na Geofrey Stephen Arusha
Wiki ya Asasi ya Kiraiya imeendelea na vikao vyake Jijini Arusha ambapo leo mapema wametembelea soko la kilombero Jijini Arusha na kutazama namna wanawake wanavyo jishughulisha na biashara zao za huuzaji ,Mboga mboga matunda na mahitaji mengine mbali mbali muhimu kwa wananchi.
Akizungumza na Arusha24Tv Deo Bwire wakili wikili kutoka Asasi ya Kiraiya amesema malengo ni kutembelea soko hilo ni pamoja na kusaidia wanawake watoto wa kike katika kutatua changamoto zinazo wakabili katika maswala ya ukatili wakiwemo masokoni ambapo asilimia kubwa ni wanawake.
Amesema ziara kama hizo ni muhimu katika kutambua changamoto zao hususani kero za soko ikiwemo miundo mbinu ya soko hilo ambapo pia imebainika kutokuwepo vikao vya maendeleo ya soko ambavyo wafanya biashara hao wamesema kwamba avifanyiki .
Mwanasheria Deo amesema viongozi wa masoko wanapaswa kuwejiwekea utaratibu kutatua changamoto zinazo wakabili wanawake katika kufanya biashara zao kwani kufanya hivyo kuna tatua changamoto za ufanyaji wa biashara katika ustadi wa hali ya juu.
Naye Jane Magigita amesema wameamua kufanya ziara hiyo katika soko la kilombero Jijini Arusha kwa lengo la kujifunza kuona maisha ya wanawake watafutaji wanao amka asubui na mapema katika kutafuta maisha huku wengi wao wakiacha familia zao nyumbani na wengine kubeba watoto mgongoni kutafuta maisha kwa kufanya biashara sokoni .
Amesema wamekutana na wanawake wengi ambao wanafanya biashara zao katika soko hilo wameeleza changamoto zao kubwa ni pamoja na viongozi wa masoko , kushindwa kukaa kwa pamoja kukabiliana na changamoto zinazo wakabili ikiwemo kuunganishwa madaraja ya wanawake wafanya biashara na wale wasio wafanya biashara ambao wengi wao ni wateja kwao .
Viongozi wa Soko hilo la kilombero Jijini Arusha wameeleza furaha yao kubwa mara baada ha kuona ugeni mkubwa wa wadau wa Asasi sizizo za seriki kufika katika soko hilo kutoa elimu na kuelimisha wanawake namna ya matumizi bora ya fedha katika biashara huku wakisema ni batua kubwa sana kwao.
Wamesema wamepokea kilio cha wanawake walicho wasilisha kwa wadau hao wa Asasi sizizo za serikali ikiwemo kero mbali mbali za kwao kushindwa kutatailiwa kwa wakati vikao kushindwa kufanyika kwa wakati na kuwahidi kuzifanyia kazi mara moja .
Mwisho