Na Richard Mrusha Salaam
MWENYEKITI wa Shirikisho la Jumuiya ya Afrika Mashariki Josephat Rweyemam Amewataka wanachama na wajasiliamali kushiriki maonyesho ya wajasiliamali yatakayofanyika nchini Burundi (Bujumbura) mwishoni mwa mwaka huu.
Amesema maonyesho hayo yanayotambuliwa kama JuAKALI Nguvu Kazi Afrika Mashariki yanatarajia kuanza Disemba 5 _ 15 na kwamba maonyesho hayo ni endelevu na yaliaza mwaka 1999.
Mwenyekiti Rweyemam ameyasema hayo Novemba 14 mwaka huu jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo Amesema ilitiwa Saini ya kuunda Jumuiya ya Afrika Mashariki na wakati huo Marais Kwa pamoja walikubali kuwepo Kwa maonyesho hayo na yatazunguka Kwa Kila nchi.
“Maonyesho haya ni ya 23 tangu kuazishwa kwake na katika maonyesho haya zitafanyika shughuli mbalimbali za siku na kutakuwa na siku ya Tanzanaia ambayo itafanyika Disemba 10 na itakuwa siku mahususi ya kuonyesha bidhaa zetu.”Amesema
Nakuongeza kuwa “Tumeshatoa fomu Kwa wajasiliamali washiriki wajaze na kuzirudisha mapema kwasababu muda si rafiki na mategemeo yetu nikwenda na wajasiliamali 300 ambao wanabidhaa mbalimbali za kusindika na nguo na masharti lazima zitengenezwe kwenye nchi husika.”amesisitiza Mwenyekiti Rweymam
Ameongeza kuwa maonyesho hayo yatakuwa na zaidi ya wajasiliamali 1000 kutoka nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki ikiwemo sauth Sudan,congo ,Rwanda ,Burundi,Kenya ,Uganda na Tanzania na kauli mbiu ya mwaka huu ni ” kuwaunganisha wajasiliamali wadogo na wakati wa Afrika mashariki kufanya biashara katika eneo la Jumuiya ya Afrika Mashariki ”
Pia Amesema wanahamasisha wajaslimali kuweza kufanya biashara katika eneo la Afrika Mashariki na maonyesho hayo yanafundisha watu namna ya kuvuka mipaka na kujua sheria na taratibu Kwa wenzao na kujifunza utalaamu kutoka Kwa wengine .
Pia Mwenyekiti Amesema wanahamasisha vijana kushiriki Kwa wingi ili kuweza kuingia kwenye ujasilimali wakiwa vijana Kwa lengo la kuongeza Ubunifu .
“Haya maonyesho yanandaaliwa chini ya Jumuiya Afrika Mashariki lakini pia Kwa Wizara na Kwa hapa kwetu ni chini ya Wizara iliyo chini ya ofisi ya Waziri mkuu Kwa maana Wizara ya kazi na ajira na maandalizi yote yapo sawa na watu wanarudisha fomu na hivi Sasa wanatafuta usafiri wa kisafirisha mizigo pamoja na washiriki .”Amesema Rweyemam
Amesema maonyesho hayo ni fursa na nivema watu wakajiandikisha ili kuweza kushiriki wasipoteze nafasi hiyo na pongezi Kwa taasisi za usimamizi na ubora wa viwango kwani wamekuwa karibu Kwa wajasiliamali na kuweza kutoa ushauri hali inayofanya wadau kuwa na bidhaa Bora zaidi na pia Kuna baadhi ya taasisi za serikali wanakwenda nao.
Akizungumzia utaratibu wa kusafiri Amesema kuwa Kuna vitu vya kuzingatia pindi unapokwenda kwenye nchi za watu kama vile mpakani inahitajika passport,lakini chanjo Kwa vijana ,chanjo ya COVID japo hivi Sasa haina nguvu ila nimuhimu kujiandaa.
Pia Amesema nivema Kujua mabadiliko ya fedha kati ya fedha ya kule na ya kwetu ili kujiandaa Kwa lengo la kukwepa changamoto.
Naye mratibu mkuu wa maonyesho hayo ya JUAKALI Nguvu Kazi Zubeda Omar Amewataka wajasiliamali kujitokeza kuchukua fomu na kwenda kushiriki na watakaojitokeza kwenda nchini Burundi kuacha kuzungumzia mambo ya nchi yao bali wakafanye jambo ambalo limewapeleka.
Akizungumzia mwitikio wa uchukuaji fomu Zubeda Amesema mwitikio ni mkubwa na wengi wamechukua fomu hivyo jambo kubwa Kwa wajasiliamali wajiandae Kwa fedha ya Akiba lakini pia Kwa wale wenye magonjwa kama kisukari na magonjwa mengine wakumbuke kubeba dawa zao.