Dkt Mahera ameyasema hayo jijini Arusha wakati akifungua mafunzo ya wiki mbili kwa wakuu wa vyuo vya afya vya serikali kutoka mikoa mbalimbali nchini yanayofanyika katika chuo cha Afya cha CEDHA.
Aliwataka wakuu wa vyuo kufundisha wahuduma wa Afya namna ya kujali wagonjwa, akili hisia na uwajibikaji.
Katika hatua Nyingine dkt Mahera alisema serikali imejikita kuwekeza katika sekta ya Afya kwa kuweka vifaa tiba, ujenzi wa za zahanati takribani 6000,ujenzi wa vituo vya afya kutoka 400 hadi 755 na wamejipanga kujenga vituo vingine vya afya vipatavyo 214 mwaka ujao 2024.
Awali mkuu wa Chuo hicho cha Afya cha CEDHA Dkt Johannes ,Lukumay,alisema kuwa mafunzo hayo yamekuwa na mwitikio mdogo Kutoka Katika timu za usimamizi na uendeshaji wa huduma za afya kuanzia ngazi ya taifa hadi halmashauri Vituo vya kutokea huduma za afya na Vyuo vya afya Nchini.
Alisema kuwa mafunzo hayo yanawalenga Viongozi wa Sekta ya afya ngazi mbalimbali kuanzia makao makuu ya Wizara ya afya ofisi ya Rais,Tawala za mikoa na Serikali za mitaa,Wakuu wa Vyuo vya afya na wasaidizi wao,waganga Wakuu wa mikoa ,hospitali za rufaa za mikoa pamoja na timu za uendeshaji wa huduma za afya ,waganga Wakuu wa Wilaya na waganga wafawidhi wa Wilaya pamoja na timu zao za uendeshaji huduma za afya na Vituo vya kutolea huduma za afya.
Alisoma Ili kuimarisha utawala bora,Uongozi na manejimenti ya usimamizi wa huduma za afya Kwa kushirikisha Kamati za Ulinzi na Usalama na Viongozi na watendaji wa Serikali katika ngazi za Viongozi Wakuu wa halmashauri,wakiwemo Wenyeviti na Wakurugenzi wapatiwe mafunzo ya manejimenti,Uongozi na utawala Ili kuwepo uelewa endelevu wa pamoja katika kusimamia na kuendesha huduma bora za afya kwa ngazi ya msingi.
Mwisho .