Serikali imekipongeza chuo cha Uhasibu Arusha kwa kuja na mabadiliko ya mitaala ya elimu katika upande wa kilimo, Biashara ,ufundi,utalii ambayo kwa kiasi kikubwa inayoakisi mazingira halisi ya kuisaidia Tanzania katika ukukuzaji wa uchumi.
Akiobgea katika mahafali hayo Naibu Waziri wa Kilimo, David Silinde ameyasema hayo kwa niaba ya Waziri wa fedha wakati akizungumza katika mahafali ya 25 ya Chuo cha Uhasibu Arusha yenye wahitimu 5387 yaliyofanyika Katika hoteli ya Ngurdoto wilaya ya Arumeru mkoani Arusha.
Amesema serikali imewekeza fedha nyingi katika vyuo vya elimu ya kati na vyuo vikuu, kutokana na jitihada kubwa zinazofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha watanzania wanapata elimu bora na yenye usawa.
“Nafahamu kila mmoja amefanya tafiti kama takwa la chuo kabla ya kuhitimu, ni imani yangu kila mhitimu aishirikishe jamii yake ,na kutokufungia matokeo hayo kabatini, tumieni utafiti mlioufanya ili kuongeza tija katika mabadiliko yakiuchumi.”amesema .
Kwa upande wake Mkuu wa chuo cha uhasibu Arusha (IAA) Profesa Eliamani Sedoyeka amesema chuo icho kwa sasa kina jumla ya kozi 71 ambapo 16 stashahada, 17 stashahada, uzamili 14,shahada 24 .
Ameeleza chuo kimeanzisha shahada mpya ya medua bainowai na mawasiliano ya umma, kutokana na mazingira ya Sasa kupitia msisisitizo wa serikali katika sekta ya elimu yakutengeneza kada ya viongozi katika eneo hilo katika usimamizi wa shule na maafisa elimu ngazi ya wilaya .
“Serikali iliwapatia chuo hiki shilingi 48 bilioni na mipango ni kukakikisha chuo kinatoa misingi ya weledi na umahiri na kuwa kinara katika maeneo yote , huku mipango mikakati ya miaka 5 ni kuongeza wigo wa kujenga miundombinu ya kufundishia,kituo cha tehama, kumbi pacha za kufundishia katika kampasi 4 ya Arusha,Babati, Dar es salaam, Dodoma na tuna mpango wa kuanzisha kampasi nyingine mpya ya Songea ambapo tayari tumepatiwa shilingi 22 bilioni na serikali kwa ajili ya kujengwa kampasi hiyo ili kutengeneza soko lenye uhakika.”amesema.
Hata hivyo ili kuhakikisha usalama wa Raia na mali zao zinalindwa wameimarisha mahusiano na chuo cha polisi Moshi kwa kuja na kozi mbalimbali kwa lengo la kuvifikia vyombo vya ulinzi na usalama.