Na Doreen Aloyce, Dodoma
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt, Ashatu Kijaji (MB) amezitaka Taasisi zinazohusika na utoaji Leseni(Brela) Shirika la Viwango Tansania (TBS) na wakala wa vipimo sahihi (WMA)kupita kwenye viwanda vyote nchini vinavyo zalisha bidhaa za mabati na bidhaa nyingine kukagua na kujiridhisha kama bidhaa zinazozalishwa na viwanda nchini zinakidhi vigezo vilivyo ainishwa na kukubalika na Serikali.
Waziri Kijaji ameyasema hayo leo 22 febriari ,2024 jijini Dodoma wakati alipofanya ziara katika kiwanda cha kuzalisha mabati cha ALAF na Herosean Interprises inayozalisha mabati ya DRAGON ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha uwekezaji wa Viwanda unaboreshwa hapa nchini.
Aidha waziri akiwa kwenye ziara hiyo kwenye kiwanda cha Herosean Interprises kinachozalisha mabati ya DRAGON ameweza kubaini uwepo wa bidhaa nyingine ambazo haziusiani na malengo halisi ya leseni iliyotolewa na BRELA.
“Leo nimetembelea viwanda hivi viwili lakini cha kusikitisha hiki kiwanda cha kuzalisha mabati ya DRAGONI kinajihusisha na biashara mbalimbali ikiwemo Friji, PVC, Vigae na Gypsum Bord na nikawataka wanioneshe vielelezo vya usajili wa bidhaa hizo wameshindwa kuonesha mpaka naondoka sipati jibu sahihi”Amesema Dkt. Kijaji ”
Pia Waziri Dkt.Kijaji amevitaka viwanda kuuza bidhaa za mabati zinazozalishwa na viwanda hapa nchini kuuzwa kwa bei rafiki kwa wanunuaji kwa makundi yote.
” Jambo lingine ninalotaka kuwaambia watanzania kwa bidhaa nilizotembelea leo ,ukilinganisha kwa nchi za Afrika mashariki kwa bidhaa hii ya mabati sisi Tanzania bei yetu ipo chini kuliko nchi yoyote ile ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki hivyo niwatake msisikilize kelele za mtaani endeleeni kujenga kwa wingi na sisi kama Serikali tunaendelea kutekeleza miradi yetu”Ameongeza Dkt. Kijaji.
Kwa nyakati tofauti, wazalishaji wa viwanda hivyo Herry Jailos afsa huduma kwa wateja kiwanda cha mabati ya Alaf na Boniface Lekwasa Afsa Masoko Kiwanda cha kuzalisha mabati Dragon
wameishukuru Serikali kufanya ziara na kubaini changamoto zinazowakabili ikiwemo ukosefu wa masoko kutokana na wazalishaji wa bidhaa hizo kuwa wengi.
Mwisho .