Mwandishi wetu,Arusha.
Wakulima zaidi ya 300 kutoka mikoa ya Geita Iringa Mbeya Morogoro Mwanza Shinyanga na Tabora wametakiwa kuacha tabia ya kununua mbegu minadani badala yake wanunue katika mawakala waliosajiliwa.
Akizungumza katika mafunzo ya wakulima yaliyotolewa na wataalamu wa sayansi ya mimea wa kampuni ya Balton Tanzania inayoingiza na kusambaza mbegu nchini Tanzania Afisa Mfawidhi wa taasisi ya Kuthibiti Ubora wambegu Tanzania, Kanda ya Kaskazini, Dk Munguatosha Ngumuo alisema ni muhimu kununua mbegu zilizothibitishwa.
Dk Ngomuo alisema wakulima wanapaswa kuacha kilimo cha mazoea badala yake wajifunze kulima kisasa kwa kutumia mbegu bora ambazo zimethibitishwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Balton Tanzania Chris Keeping aliwataka wakulima hao kuwa kufahamu aina ya mbegu inayofaa kulima katika ukanda waliopo pamoja na kujifunza namna ya kudhibiti wadudu kuwasaidia kupata mazao mengi Kwa wakulima hao.
Amesema kuwa kufanya kilimo chenye tija hususani kipindi hiki cha athari ya mabadiliko ya tabia ya nchi kutapelekea kuwa na chakula cha kutosha nchini na ziada kuuzwa nchinza nje.
Mtaalamu wa sayansi ya Mimea wa BaltonTanzania Halima Amir alisema wakulima wanatakiwa kutumia mbegu sahihi na kulima kwa kuzingatia utaalam.
Wakulima Paulo Nko wa Ngaramtoni wikaya ya Arumeru na Hapiness Kaweji kutoka Tarakia mkoani Kilimanjaro walipongeza elimu iliyotolewa na Balton katika kuboresha kilimo chao.
Mafunzo hayo ya siku tatu yanatolewa na kampuni ya kuuza mbegu ya Balton Tanzania ambayo pia yameshirikisha mawakala wa mbegu nchini na wataalam wa kilimo.
Mwisho