Mbunge wa Hai (CCM), Saashisha Mafuwe amesema Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imefanya mambo mengi jambo ambalo wanauhakika katika chaguzi zijazo watafanya vizuri.
Haya ameyasema wakati wa ziara Katibu Mkuu wa Chamacha Mapinduzi (CCM)Dk Emanuel Nchimbi Wilayani Hai katika muendeleze wa ziara yake kufuatilia utekelezaji wa ilani,kusikiliz kero za Wananchi na kuangaza maandalizi ya chaguzi zijazo.
Mafuwe amesema katika Jimbo hilo ambalo kwa miaka mingi limekuwa likiongozwa na upinzani amedai haikupata maendeleo. Miongoni mwa wabunge walioongoza ni Freeman Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema.
“Tulikuwa na watu hapa miaka 25 hatukuona walichokifanya, leo maendeleo ambayo tumayafanya ni historia ndani ya Wilaya ya Hai, tupelekee salamu kedekede kwa Mama Samia kwa mambo ambayo ameyafanya.
Nilisimama hapka nikawaambia wananchi wa Hai, suala la maji yatakwenda kupatikana, niliipiga kelele kwelikweli bungeni miongoni mwa wabunge wanaouzungumza zaidi bungeni ni mimi Saashisha Mafuwe,” amesema Mafuwe.
Amesema kwa sasa tatizo la maji Bomang’ombe limekwisha, tulipewa Sh3.39 bilioni katika mradi wa maji na kuna mradi mkubwa kule Mkalama unaendelea, tunahakikisha maji yanapatikana ya kutosha.
Pia amesema kuhusu sekta ya afya, amesema Hospitali ya Wilaya ilisahaulika lakini kwa sasa kuna Chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU):”Imejengwa mpya, leo tuna jengo la mama na mtoto limejengwa na magari mawili ya wagonjwa.”
Mbunge huyo amesema sekta ya elimu imepiga hatua huku akiomba kuwa shule nyingi zimejengwa tangu mwaka 1952 nyingi ni chakavu kimebaki kipande kidogo tu, najua hili Katibu Mkuu najua utamaliza.
Kuhusu hili, Dk Nchimbi ameitaka Wizara ya Elimu na Tamisemi kufanya utafiti wa shule zote chakavu ili kuzifanyia maboresho ili ziwe katika mazingira mazuri.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu amesema Serikali imeleta Sh829 bilioni ndani ya miaka mitatu za utawala wa Rais Samia ulioingia madarakani Machi 19,2021 zimepelekwa mkoani humo kwa ajili ya miradi mabalimbali ya maendeleo.
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla amesema mwaka huu tutakuwa na uchaguzi wa serikali za mitaa na mwakani kutakuwa na uchaguzi Mkuu, kwa haya mambo mazuri ambayo Rais Samia amefanya tunaomba muendelee kutuamini, itakapofika uchaguzi tuwachague viongozi wa vijiji wenye Bendera ya CCM.
“Tunataka tushinde uchaguzi wa serikali za mitaa kwa kishindo, ili tuwapelekee salamu kwamba mwakani tutachukua udiwani, ubunge, na Rais wetu mama Samia Suluhu Hassan. Tuendelee kuhamasishana mafanikio haya tulipopata ni kwa sababu ya mipango mizuri ya Chama cha Mapinduzi.
Mwisho