Na Geofrey Stephen Arusha .
mafunzo ya ujasiriamali wa kuzalisha bidhaa mbalimbali yanayotolewa kwa vijana na walezi ikiwa ni hatua ya kuwezesha jamii kujitafutia kipato ili kumudu malezi ya watoto.
vijana na walezi hao ni zaidi ya 1000 mkoani arusha wamekusanywa kwa pamoja na wameanza kupatiwa mafunzo ya ujuzi wa ujasiriamali kupitia shirika la viwanda vidogo dogo nchini sido kwa kushirikiana na taasisi ya sos pamoja na wadau wengine kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kiuchumi.
meneja wa sido mkoa wa arusha jalphary donge akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo amesema mpango huo wa awamu ya kwanza imejumuisha vijana na walezi wapatao 300wakiwemo vijana wakiume na wakike ambao wanapatiwa mafunzo ya kuzalisha bidhaa mbalimbali kwa matumizi ya kijamii .
kwa upande wake katibu tawala msaidizi wa mkoa wa arusha anayehusika na viwanda,uwekezaji na biashara frank mbando amesisitiza vijana kutumia vyema fursa zinazotolewa ili waweze kukuza uchumi wao na uchumi wa taifa kwa kuzalisha bidhaa zenye ubora na zenye kukidhi maitaji ya kila siku .
kwa upande wake mratibu wa uwezeshaji wa familia na vijana kutoka shirika la sos la mkoani arusha bwana willson rando amesema maradi huo unafanya kazi ya malezi mbadala kwenye jamii ,kusaidia vijana kujikwamua kiuchumi pamoja na utoaji wa mafunzo ya ujasiriamali.
amesema wao ni miongoni mwa waezeshaji wa mafunzo hayo kwa vijana kujikita kufanya shughuli za ujasiria mali kwa lengo la kupata ajira na kujiongezea kipato nankuakisha wanakua na uwakika wa kunudu majukumu ya familia pamoja na kujiongezea kipato cha kila siku
mwisho .