Na Bahati Siha .
Mkuu wa Wilaya Siha mkoani Kilimanjaro Christopher Timbuka ametaka Wananchi Wilayani humu kuchukua tahadhari kuhusu ugonjwa wa homa nyani unaujulikana(MPOX)
Haya ameyasema alipopewa nafasi ya kutoa pole nyumba kwa Diwani wa kata ya Sanya juu Juma Jani Baada ya mazishi ya make wa Diwani huyo,ambapo yalihudhuria na Viongozi mbalibali wa Chama ,Dini, Serikali pamoja na madiwani.
Akizungumza Mara baada ya kupata frusa hiyo ameitaka jamii kuzigatia kwa kuchukua tahadhari za wataalamu wa Afya ,baada ya hapo kuna vikao mbalibali vitafanyika timu ya Afya,ili Wananchi wote waweze kuchukua tahadhari
Amesema tahadhari ya kwanza ni zile zile tulizokuwa tunazitumia wakati wa ugonjwa wa uviko 19 ,najua ni utamaduni tumezoea kupeana mikono,kukumbatiana
Kwa hiyo naomba sana ,tuanze kuchukua tahadhari hizo,kama tulivyokuwa tunachukua kipindi cha uviko 19,
Timbuka amesema moja wapo ni kwamba katika sehemu zote za mikusanyiko au hata majumbani kwenye kaya , lazima tuwe na vifaa vya kunawia mikono.
Amesema ndugu zangu tuanze ,Nchi jirani ya Kenya sio mbali kutoka kwetu na watu,tunamuingiliano sana, Kenya kuna visa 2 mpaka sasa, Tanzania walikuwa wanaisiwa watu wawili
Lakini bahati nzuri tunamshukuru Mungu haikuwa hiyo bado haijaingia,lakini tunafanyabiashara sana ,tunawatembelea wenzetu wa Kenya na pia tunaenda Nchi ya Kongo ,Kongo sio mbali sio mbali.
“Tunaomba sana tuchukue tahadhari kwenye ugonjwa huu ili usiweze kuingia na kubwa tunaloomba ,wale watu watakao onyesha dalili za ugonjwa huu basi tuwafikishe kwenye vituo vya Afya”amesema Timbuka
Na wenzetu wa Afya watafanya yale walioelekezwa,Kwa hiyo kama tutapita Maeneo mbali mbali naomba tuzingatie swala la ugonjwa huu
Mmesikia mmeona kwenye vyombo vya habari dalili ikiwamo pamoja na kutoka upele na malenge lenge ,lakini sisi kama Nchi lazima tuchukue tahadhari ili usiingie kwetu na ukiingia tunaweza kuuthibiti mapema nawasii sana kwenye hilo
Kwa upande wake Immamu wa Misikiti wa SanyaJuu Aly Muhammad, naye Akizungumza amewataka jamii kuendelea kufanya mambo mema yanayompendeza Mungu
Amesema wapo watu hawana hofu ya Mungu,wanafanya mambo yasiyompendeza kwenye jamii wanafanya ukatili ikiwamo,ubakaji na ulawiti haya mambo tuyakemee Kwa nguvu zote tusikae kimya kwani ni chukizo ili jamii ibaki salama
Awali Diwani huyo aliwshuku Wananchi wote waliomkimbilia katika kipindi kingumu na kumfariji bila kumsahau Mubunge wa Jimbo hilo Godwin Mollel kwa njisi alivyo msaidia wakati akiwa na mgonjwa hospital ya rufaa ya Kcmc.
“Ni kweli ukitaka kumshukuru mtu mshuru mbele za watu,amenisaidia,Ila hapo hapo hospital kuna mambo serikali iangalie sana “amesema Jani
Mwisho