Na Bahati Siha,
Wadau wa mazingira Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro, wamesikitishwa vibali vya kukata miti vikitolewa kwa wingi mitaani ,uku uhamasishaji wa upandaji miti kufidia iliyokatwa ukiwa mdogo
Wakimuomba Mkuu wa Wilaya hiyo Christopher Timbuka kufutilia utoaji wa vibali hivyo ili kunusuru Wilaya kugeuka jangwa.
Wadau hai wakizungumza na waandishi wa habari Kwa nyakati tofauti,Wamesema wamekuwa wakiona miti ikikatwa sehemu mbali mbali lakini hawajaona miti ikipanda kufidia iliyokatwa katika maeneo hayo
“Ni kweli ukipita sehemu utaona miti imekatwa kwa wingi ,lakini hauwezi kuona miti iliyopandwa kufidia hiyo iliyokatwa”Wamesema Wadau hao
Michael Jackson mmoja ya wadau hao ,amesema kwa muda mrefu ameona miti ikikatwa kwa matumizi ya mbali mbali ikiwamo kupasua mbao kwa ajili ya ujenzi ,lakini ukifuatilia unaona ule utaratibu tuliojiwekea ukikata miti inatakiwa upande mingine haufutwi
kitendo hicho kitasababisha Wilaya kugeuka jangwa kutokana na miti hiyo kukatwa bila kufuata utaratibu unataka kupanda miti kufikia miti iliyokatwa angalau 5 na kuendelea
“Ni kweli utaratibu uliopo unataka miti ikikatwa ipandwa mwingine ,lakini utaratibu huo hauzingatiwi ,bila kupaza sauti kukemea jambo hili Wilaya itageuka jangwa “Wamesema
Joyce Mmari mkazi wa kibongoto Wilayani humo , ametaka wanaotoa vibali Kwa ajili ya kukatwa miti wanatakiwa kuchunguzwa ,kufuatiliwa vinginevyo watatusababishia majanga kwa kutanguliza maslahi yao mbele na kuacha mazingira yakiharibiwa
Raisi Samia Suluhuu Hassani Kila siku anasisitiza kutunza mazingira ikiwa kupanda miti ,lakini hawa wanatia vibali wanamuangusha Rais kufikia malengo aliyekusudia ya utunzaji mazingira
Mmari amesema ukipita Maeneo ya kata ya Evae’ny , Kashashi,Livishi,na kirua miti imekatwa kwa wingi ,lakini iliyopandwa hakuna ,kwa kweli hawafanyi vizuri
Tena ukichulia Kuna Viongozi wa Serikali wapo maeneo hayo,wapo watendaji wa kata,vijiji ambapo walitakiwa kukemea mambo hayo, lakini wao wapo kwa maslahi yao badala ya kuwa jicho la Serikali,hawafai kuwa watumishi
“Ni kweli wapo watu walioajiriwa kwa ajili ya mazingira iweje mazingira yanaharibiwa na wao wapo,kama haya mambo yataendelea hatutakubali tutaandamana hadi kwa Rais Samia Suluhuu Hassani kumuekeza uharibifu huo wa mazingira “amesema Mmari
Kwa upande wake Zakayo Mushi ,amemuomba Mkuu wa Wilaya kuunda timu ya kufutilia utunzaji mazingira ndani ya Wilaya hiyo,ikiwamo kwenye vyanzo vya maji ambao watu wanalima ndani ya miti 60 kinyume na utaratibu na utoaji vibali vya ukataji miti kama unazingatiwa
Lazaro Mwaruko Afisa misitu Wilayani humo, amesema vibali hivyo vinatolewa na Viongozi wa vijiji Kwa kupewa barua na kuja kwetu
Kwa hiyo akija na hiyo barua kwamba tukijiridhisha inatoka kijijini kwa utambulisho wa mihusika tunamruhusu,ikiwa miti msingi sana inatulazimu tuende,lakini kuanzia miti 5 kushuka chini tunaamini Ile barua.
Ila hilo la ukataji miti na upandaji miti tunazingatia sana,kwa sasa hatuwezi kupanda miti hadi mvua inyeshe haiwezi kukua
Mwisho