Na Bahati Hai
Vibaka wawatishio Kwa wakazi wa Bomang’ombe Baadhi yao waacha kwenda kazini kwa kuhofia nyumba zao kuvunjwa na kuibiwa mali zao
Hai, Wananchi wa kata ya Bomang’ombe,Muungano na Bondeni Wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, wanaoishi kwa wasiwasi baada ya kuzuka wimbi la wizi linadaiwa kufanywa na vibaka nyakati za mchana na usiku na wanalazimika kubaki majumbani ili kuwa walinzi
Vibaka hao wamekuwa wakifanya wizi huo kwa njia tofauti tofauti ikiwa ni pamoja na kuwapora kina mama simu na fedha wanapokwende sokoni nyakati za asubuhi alifajiri ,pia watumishi na Wafanyabiashara wanapokwenda kwenye shughuli zao wanaporudi jioni wanakuta nyumba zao zimevujwa na kuibiwa vitu mbali na hao vibaka
Wakiomba Polisi kata kutoa elimu kwa Wananchi namna ya kupambana na vibaka hao ikiwa pamoja na Polisi kuweka doria nyakati za chana na usiku kwani wanasababisha kurudisha maendeleao nyuma
Wakizungumza na waandishi kwa nyakati tofauti ,baadhi ya Wananchi hao Wamesema kwa sasa wameacha shughuli za kwenda kujitafutia kipato ,wakihofia wakiondoka nyumbani vibaka watavunja kupora vitu.
“Ni kweli tunaishi kwa wasiwasi ,njiani ukiwa unatembea wanaweza kujitokeza wakakupora mkoba na simu, wakatonea ,nyumbani tena unapondoka wanaweza kuvunja na kuiba kwa hiyo ni hatari tunaishi kwa wasiwasi ,ndiyo maana tunaomba Polisi kata watujengee uwezo “Wamesema Wananchi hao
Asia Suleimani mkazi wa Gezaulole ,amesema alikuwa amelala nyakati za usiku ambapo alistuka dirisha likiwa wazi nakubaini kwamba simu na fedha zimechukuliwa kwa kuvunja vitasa vya dirisha
Asia anasema vijana hao wanatembea na silaha za jadi ikiwamo Rungu,kisu ,nondo, panga ukikutana nao wanakupora vitu nakutokomea ,pia wanakuwa na ubao mrefu uliopakwa gundi ,wakifanikiwa kufungua dirisha wanaingiza huo ubao ndani wenye gundi ndani yenye fundi na kuchukua vitu kama simu fedha
Amesema ili ni tukio la 30 ndani ya wiki mbali katika mtaa huu wa Gezaulole,madirisha yanavunjwa ,wanachukua simu na fedha, sehemu nyingine wanavunja hata mchana ,Kwa kweli tumechoka vijana sio kwamba hawajukikani wapo mtaani hapa Viongozi waangalie swala hili
Wakati mwingine unashindwa kwenda kutafuta ridhiki unabaki nyumbani kulinda kilichopo,unaweza kwenda kutafuta ridhiki unaporudi nyumbani unakuta wameshakuibia Kila kitu,tunaomba Polisi kata watusaidie kutoa elimu ikiwa ni pamoja na kufanya Doria
Messe Ndosi mkazi wa Mtaa huo, amesema yeye ni muhanga wa jambo hilo,kwani November 6 mwaka huu majira ya saa mbili usiku akiwa ametokea katika shughuli zake,aliporwa nyaraka zake pamoja na simu na vijana walikuwa kwenye pikipiki ,hii tabia imekuwa kubwa ,hatuna Imani tunatembea Kwa wasiwasi
Kwa upande wake Jemsi Munuo mkazi wa Magadini Wilayani humo, amesema ukiachana na wezi wa simu na fedha unaofanywa na hao vibaka pia kuna wezi wa kuku ,umefuga lakini wanakuja kukuibia hii ni kurudisha maendeleao nyuma kwa Wananchi inakatisha tamaa
Julius Swai mkazi wa mtaa Bomani,ambaye pia ni Mwenyekiti aliyemaliza muda wake,amesema kumekuwa na hali ambayo sio nzuri wamejitokeza vijana kwa kasi kipindi hiki ambacho Viongozi wa Serikali za mitaa hawapo madarakani
Kumekuwa na wizi wa mchana,watu wanadaiwa ni vibaka wanaingia kwenye nyumba,sanasana nyumba ambazo zinaukuta,watu ambao wamezungushia ukuta, wanaingia Kwa kuruka ukuta,wanaingia na mikasi wanakata madirisha wanachukua vitu vya ndani ikiwamo tv,radio,fedha na simu
Wananchi wachukue tahadhari,asilimia kubwa wanakaa katika eneo hili ni watumishi na wafanyabiashara wanapotoka kwenye majumba yao wasiweke Imani kwenye ukuta walizungushia nyumba zao ,bali wahakikishe wanawaaga majirani hii itasaidia kidogo
Pia wezi unafanyika saa kumi na mmoja asubuhi vibaka wanafahamu kina mama uwa wanaenda sokoni Sadala wanawahi mizigo ya Asubuhi Kwa ajili ya biashara zao
Nawashauri wasiende mmoja mmoja wakinyanyuka waambizane ili waongozane wawe wanna au watano ,anapokuwa mmoja ni raisi kukutana na kubaka na kumkwepulia simu na fedha au vitu vingine
Mkuu wa Wilaya hiyo lazaro Twange, Akizungumza kuhusu swala hilo,ameahidi kulifanyia kazi.
Nashukur kwa taarifa ,nikuongeza doria kwenye maeneo hayo,kwa kushirikiana na Viongozi au watu maarufu wa maeneo hayo
Mwisho