Na Richard Mrusha
WAZIRI mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye kongamano la Kimataifa namba 14 litakalofanyika tarehe 4 Desemba mpaka tarehe 6 Desemba mwaka huu kwenye ukumbi wa kimataifa Arusha(AICC) jijini Arusha.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi mtendaji ya Taasisi ya Wahandisi Tanzania(IET),Ipyana Moses ,
Amesema kongamano ilo litawashirikisha wahandisi,mafundi,wanafunzi na wadau wengine kutoka mikoa mbalimbali nchini na nje ya nchi.
“Umuhimu wa kongamano hilo ni kukutana na washiriki na tunakadiria kuwa na zaidi ya elfu moja, na katika hao wako watakao shiriki kwa njia ya mtandao amesema Moses.’
Moses amesema dhima ya kongamano hilo ni kukuza na kufanya Ubunifu,Uhandisi bora katika Dunia inayobadilika” huku kongamano linatarajiwa kuwa na mawasilisho ya mada zilizochaguliwa kutoka kwa wawasilishaji wabobezi katika tasnia ya Uhandisi.
“Katika kongamanoni mada zitajikita katika kutoa elimu bunifu na zinalenga kuhimiza na kuchochea ari ya kuondoa dhana ya ufanyaji kazi wa kimazoea na kusisitiza ubunifu”Amesema
Moses amewataka wahandisi na wadau wote wa sekta mbalimbali za uchumi nchini kwenda kushiriki kwenye komgamano hilo huku akiwakumbusha wahandisi na mafundi ambao hawajajiunga na taasi ya (IET)wajiunge na taasisi hiyo.
Amesema uhandisi ni kitovu cha maendeleo katika sekta zote na wanaona miundombinu yote ikiwemo barabara reli ya kisiasa na NK hizo zote ni kazi za kihandisi hivyo huwezi kuikimbia.
Ameongeza kuwa Mchango wa uhandisi ni mkubwa ndiyo maana waanafanya hayo makongamano kwa lengo la kukuza ubunifu kwa wahandisi ili waendane na teknologia ya kisasa kwasababu dunia ya sasa inaenda kasi na vitu vinabarika kila siku.
Mwisho..