Siha,
Wananchi Wilayani Siha Mkoani Kilimanjaro wametakiwa kujitokeza katika maadhimisho ya juma la Sheria ili kupata elimu itakayo wasaidia kufahamu haki zao za msingi pindi wanapopata matatizo mbali mbali ikiwamo yakufanyiwa dhuluma
Kauli hiyo imetolewa na Idrisa Mndeme Makamu Mwenyekiti wa Jumuhiya ya maridhiano na Amani Tanzania (JMAT),Wilaya ya Siha mkoani hapa, wakati wa uzinduzi wa maadhimisho haya yaliyofanyika soko la SanyaJuu Wilayani humo.
Akizungumza mara baada uzinduzi huo,amewataka Wananchi kutumia frusa hiyo inayowafanya watamvue haki yao ya msingi
“Wananchi hii ni wiki ya Sheria jitokezeni kwa wingi kwenye maeneo yenu yaliyotajwa ili mpate frusa ya kuuliza na kujua nini linaendelea katika sheria,itasaidia kufahamu haki zenu ili kuepuka kuonewa kwa kutokufahamu amesema Mndeme
Mndeme amesema watu wengi hawaelewi haki zao , hivyo kusababisha wakati mwingine kufungwa au hata kupoteza mali zao hivi hivi,kwa hiyo kupata elimu kunaweza kuwasaidia
Kwa upande wake Salome Munuo mkazi wa West Kilimanjaro,ameomba elimu ya Sheria iendele kutolewa kwa Wananchi hata kwa mwezi mara moja Kwa kila wilaya sio kusubiri mpaka maadhimisho ya wiki ya sheria
“Wakati mwingine unakumbana na mtu ambaye atakudhuluma mali unamfuata mwanasheria anakuambia leta fedha nikusaidia fedha hauna, unapoteza haki yako ,pia elimu hii itatusaidia kufahamu kumdhamini mtu kituo cha Polisi kama unatakiwa kutoa fedha au la “amesema Munuo
Awali Hakimu mkazi mfawidhi Mahakama ya Wilaya ya Siha Jasmin Abdul , Akizungumza swala hilo , amesema watatembelea maeneo mbali mbali yakiwamo shule za msingi, Sekondari na Masokoni pamoja na nyumba za ibada
Jasmin amesema mpaka sasa wameshafika soko la SanyaJuu,shule ya msingi Sanya Hoyee,shule ya Sekondari Kilingi,pia watafika shule ya Sekondari Namwai pamoja ,shule ya msingi Namwai ,soko la Ngarenairobi pamoja na Kanisa la kkkt SanyaJuu
Ameeleza Kuwa Mahakama ya Wilaya ya Siha imeungana katika kuhakikisha wiki hii ambayo imeanza Tarehe 25 ya mwezi wa kwanza kutembelea Maeneo Mbali Mbali kwaajili ya utoaji Elimu .
Aidha amesema Wananchi wanatakiwa kujitokeza katika Maeneo hayo kwani Elimu inayotolewa hapo ni
bure na watakuwa na nafasi ya kuonana na wataalamu Mbali mbali wa Sheria kwenye maeneo tofauti tofauti ambapo watakuwa na uwezo wa kueleza changamoto wanazokutana Nazo za kisheria
Mahakama ya Tanzania ina adhimisha Wiki ya Sheria ambayo rasmi ilizinduliwa Junuary 25 2025 Ambapo kilele chake kinatarajiwa kufanyika February 3 2025.
Maadhimisho hayo yanaenda na kauli mbiu inayosema Tanzania ya 2050, Nafasi ya Taasisi zinazo simamia
haki madai katika kufikia Malengo makuu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo .
Mwisho