Siha,
Taasisi mbali mbali za kupinga vitendo vya ukat
ili ikiwamo ubakaji na ulawiti Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro,Wametakiwa kupambana zaidi katika kutoe elimu ambayo itasaidia kujikinga na vitendo hivyo hasa kwa wanafunzi.
Haya yamesemwa na Jane Chalamila katibu tawala wa Wilaya hiyo ,katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Sheria Nchi
Akizungumza katika maadhimisho hayo, yaliyofanyika katika ukumbi wa Mahakama ya wilaya hiyo, ameomba taasisi hizo zikiwamo za Dini kupambana katika kutoe elimu ya kupambana na vitendo hivyo.
“Ni kweli niombe taasisi kutoa elimu tuwape mbinu watoto wetu,tuwape elimu ya kukabiliana dhidi ya vitendo hivyo ili kuwanusuru na watu waovu kizazi kubaki salama”amesema Chalamila
Chalamila amesema kumekuwa na matukio ya mengi ya ukatili yanayoendelea katika Wilaya hiyo, pamoja na jitihada kutoka taasisi mbali mbali ya kuripoti na kuzuia hali hii ya ukatili bado hali sio nzuri kwa kweli
Kutokana na hali hii lazima tujitahidi kumbuni mbinu mpya ya kupambana na vitendo hivyo ikiwa ni pamoja na kuweza zaidi katika kutoa elimu,hatuwezi kukaa kimiya kuvumbia mambo hayo
Amesema katika nyumba za ibada, niwasii Viongozi wetu kutumia muda mwingi kuelezea swala hili la kupinga utatili,kwa sababu Wananchi wengi wanaamini Viongozi wa Dini.
Lakini pia nichukue frusa hii kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hii Christopher Timbuka kutoa wito kwa wazazi na walezi na jamii kwa ujumla kuwa tayari kutoa taarifa za matukio hayo ili kuokoa vizazi vyetu,wanapoona matukio watoe taarifa mara moja ili hatua ziweze kuchukuluwa
Janeth Mvungi Hakimu wa mahakama ya mwanzo Wilayani humo, amesema katika wiki ya Sheria,walitembelea maeneo mbali mbali ikiwamo shuleni na Masokoni na kwenye nyumba za ibada kutokea elimu hiyo ya Sheria
Amesema elimu waliyoitoa wiki ya Sheria haiishii hapo na kwamba Mahakama ya wilaya hiyo kila alhamisi inautaratibu wa kutoa elimu mbali mbali za kisheria katika ukumbi wa Mahakama hiyo bure ,hivyo kuwaomba Wananchi kufika hiyo siku iliyotajwa kwa kila wiki.
Hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo Jasmine Abdul pamoja na kila alhamisi kuwa na elimu ya Sheria katika mahakamani hiyo ,pia amesema watakuwa wanatembelea kwenye nyumba za ibada Kanisa na Msikiti kwa kutoa elimu ili kila mtu afahamu haki zake ikiwamo za kupinga ukatili.
Mwisho