Na Geofrey Stephen Monduli Arusha
Mapema leo Familia ya Eduard Ngoyai Lowassa ikiongozwa na Mama Regina Lowassa wafanya Misa ya shukurani katika Kanisa la Kiinjili Kilutheri la Tanzania Dayosisi ya Kaskazini KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati Jimbo la Maasai Kati, Usharika wa Monduli.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene ameungana na wanafamilia, viongozi wa chama,Serikali na wananchi katika ibada ya Shukrani ya Hayati Edward Ngoyai Lowassa Waziri Mkuu Mstaafu iliyofanyika katika Kanisa la KKKT Monduli Mjini Mkoani Arusha,
AIDHA WAZIRI SIMBACHAWENE ASHIRIKI IBADA YA SHUKRANI YA HAYATI WAZIRI MKUU EDWARD LOWASSA, Akizungumza kwa niaba ya Familia Hayati Waziri Mkuu Mstaafu Mhe.Edward Lowassa, Mwanae wa Kiume ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, Mhe. Fredrick Lowassa ametumia fursa hiyo kuwashukuru Wananchi wote waliokuwa pamoja tangu Baba yao alipofariki hadi hivi sasa huku akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mchango wake mkubwa kuwa na familia hiyo tangu Baba yao alipoanza kuugua hadi umauti ulipomkuta
Ikiwa leo ni mwaka mmoja tangu Baba yetu, Kiongozi na nembo ya Wananchi wa Monduli alipotutoka, kwa unyenyekevu mkubwa ninawaomba Watanzania wote tuendelee kumuenzi kwa yale yote mazuri aliyoyafanya enzi za uhai wake ” amesisitiza Mhe.Fredrick Lowassa
Naye, Baba Askofu Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la kilutheri Tanzania KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati Dkt. Solomon Masangwa ameitaka familia ya Hayati Edward Lowassa kuzidi kumuangukia Mwenyezi Mungu katika kila jambo wanalolifanya.
Mwisho.