Siha,
Watu wasijulikana wamehujumu miundombinu ya Tanesco Kitongoji cha Ekwenywa Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro kwa kung’oa nguzo mbili ndogo za umeme na kutoweka nazo
Wakizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti, wamesema tukio hilo limetokea February 18, 2025 na kusababisha usumbufu kwa Wananchi wa maeneo hayo
“Ni kweli upepe unapokuja zile waya zinatikisika usababisha taa kuzima na kama wapo mashine kwa ajili kushanga unga huduma inasitishwa ku to okana na moto kutotulia “wamesema Wananchi hao.
Jeremia Mollel mkazi wa eneo hilo anasema siku ya tukio aliona gari ya Tanesco likiwa na watumishi katika kitongoji hicho ,walifika na kupanda juu ya nguzo wakiwa na viatu vya kupandia
Baada ya kupanda juu ya nguzo walifungua waya za umeme wakang’oa nguzo mbili na kuondoka nazo na kucha waya zikining’inia , tulimfahamisha Mwenyekiti wa kitongoji kwamba kuna nguzo ziondolewa
Jeremia amesema baada ya muda kupitia na kuulizia imekuja kubaini kwamba watu hao hawakutumwa kuja kufanya zoezi hilo,na kwamba ni wazi wamefanye hujuma
Mwenyekiti wa kitongoji hicho Maketi Loingei , Akizungumza swala hilo,amesema mpaka sasa nguzo hazijarejeshwa na kusababisha usumbufu kwa Wananchi wamaeneo hayo
Kwani panapotokea upepo mtikisiko ukija taa zinazima ,hata kama watu wameleta mahindi kwa ajili ya kusaga watu wanakosa huduma
Maketi amesema watu hao wanasadikika wanatoka Tanesco,mtu wa kawaida hawezi kung’o nguzo zenye moto kama sio wataalamu na walikuja na gari lenge winchi na viatu vya kupandia kwenye nguzo
Wanahujumu miundombinu ya umeme wanarudisha uwekezaji unaofanywa na Serikali ,hivyo watafutwe
Kwa upande wake Meneja wa shirika hilo Wilayani Siha, Ismael Salumu amewataka Wananchi kutoa taarifa pindi wanapoona miundombinu ya Tanesco inahujumiwa ili hatua ziweze kuchuliwa kwa haraka
“Ni kweli toeni taarifaa mapema ,lakini tukio litafanyika leo inakuja kutoa taarifa kesho ni kweli jamani kwa mwenendo huu hatuwezi kufika
Mtu yeyote⁴ anaye hujumu miundombinu ya Tanesco haijalishi ni mtumishi au mtu wa kawaida tunamchukulia kuwa ni muhalifu ,tumetoa taarifa polisi
Mwisho