Moshi,
Makamishna wa Skauti mkoani Kilimanjaro wamekula kiapo ,uku wakitakiwa kufanya shughuli zao kwa kuzingatia kanuni na taratibu zilizopo kwenye katiba ili kufanya kazi kwa uaminifu
Haya yamesemwa na Halima Msangi kamishina wa Tanzania Girl Guides mkoa wa Kilimanjaro wakati wa kuapishwa makamishina hao uliofanyika katika ukumbi wa RC mkoani hapa.
Akizungumza na mara baada ya kiapo hicho, amewataka kufanya kazi za kijamii kwa mjibu wa katiba na kuzingatia kanuni za skauti inavyotakiwa
“Ni kweli ,Sisi kama skauti wa Wilaya mbalibali ikiwamo Siha na Hai tumekula kiapo kwa Mwenyezi Mungu,tumeanza na Mungu tuka muogope Mungu,tukakitendee haki kiapo hicho”amesema Halima
Halima amesema tukizingatia hayo ,tukafanye kazi kwa kila tunavyoweza ,tukisikia jambo lipo sehemu la kujitolea tusisubiri ukapewa pesa na nini kwa sababu tayari umeshakula kiapo
Amesema kanuni zipo na mmoja wapo ya kanuni kuwa muaminifu,sasa jitathimini kwamba mimi ni muaminifu,lakini pia kuna inayosema kutunza mali zangu na za wenzangu kwa sababu ya nchi yangu
Je mali za wengine unaweza au ukiona mtu anapitisha Dawa za kulevya ,sasa hivi Dunia imeharibika ukaambiwa chukua chako utakubali ,hapo lazima ulinde kiapo
Kwa hiyo tuende tukafanye shughuli za kijamii,jamii ijifunze kutoka kwetu kwa kuwa na maadili mazuri kufanya kazi kwa bidii na uaminifu,hii itafanya Taifa kuwa na watu weme na kuwa na Amani siku zote.
Abel Ntupwa Afisa Elimu mkoani hapa ambaye alikuwa mgeni rasmi kwa niaba ya katibu tawala wa mkoa,amesema kuna uuzwaji wa dawa za kulevya ikiwamo mirungi na bangi ,ulevi wa pombe kupindukia hivyo nguvu kazi ya Taifa kupungua kwenye Wilaya zenu mkasimame muhakikishi haya mambo yanaisha
“Ni kweli kiapo mlichukula mkasimamie maadili kwenye maeneo yenu,isaidieni jamii iondokane na mambo maovu ikiwamo matumizi ya dawa za kulevya ili Taifa libaki salama na liwe lenye watu wenye nguvu lenye kumpendezesha Mungu”amesema Abel
Awali kamishina wa skauti mkoa hapa Brighti Matola katika taarifa yake kwa mgeni rasmi , amesema kuna Changamoto kutoka kwa maafisa elimu Wilaya kwamba hawana fungu ,kwa hiyo mgeni rasmi watuunge mkono tunapofikisha jambo hili katika maeneo yao
Mwisho