Na Geofrey Stephen Longido
NAIBU waziri Mkuu na waziri wa Nishati Dotto Biteko amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mkuu wa wilaya ya Longido na Mkurugenzi wa halmashauri ya Longido kuhakikisha maabara ya kemia na baiolojia katika shule ya sekondari ya sayansi ya wasichana ya Longido Samia inafanyakazi haraka iwezekanavyo.
Dkt Biteko ametoa agizo hilo mapema Aprili 24,2025 katika ziara yake ya pili wilaya ya Longido mkoani Arusha,
ambapo akiwa katika shule hiyo alisisitiza kufanya kazi kwa maabara hiyo ambayo vifaa vyake vipo ila vimeshindwa kufungwa jambo lililomshangaza na kutoa siku mbili kuhakikisha inafanyakazi ili kukidhi matakwa ya serikali ya kuzalishaji wa wanasayansi wakutosha.
Shule hiyo iliyojengwa kwa zaidi ya sh,bilioni 4.4 tayari ina wanafunzi zaidi ya 300 wa kidato cha kwanza na cha tano wanasoma na imepokea baadhi ya vifaa vya maabara lakinin bado havijafungwa .
Shule hiyo iliyojengwa kwa zaidi ya sh,bilioni 4.4 tayari ina wanafunzi zaidi ya 300 wa kidato cha kwanza na cha tano wanasoma na imepokea baadhi ya vifaa vya maabara lakinin bado havijafungwa .
Akiongea huku akinyeshewa mvua kubwa na kukataa kuwekewa mwamvuki,alisisitiza kuwa serikali imewekeza katika elimu hasa watoto wa kike kwa kujenga miundombinu ya kisasa na baabara ,ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuzalisha wataalamu wa sayansi wakutosha.
SS “Nakuagiza Mkuu wa Mkoa ,Mkuu wa wilaya na Mkurugenzi kuhakikisha vifaa vya maabara vinafungwa ndani ya siku mbili ili maabara hiyo ifanyekazi na nitarudi kukagua ”
Katika hatua nyingine dkt Biteko aliagiza kufungwa kwa mfumo wa nishati safi ya kupikia inayogharimu kiasi cha sh,milioni 17 ambazo aliahidi kugharamia na alimzawadia mpishi wa jiko hilo kiasi cha sh, laki tano baada ya kuridhishwa na huduma anayotoa.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda, ameishukuru Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa katika sekta ya elimu mkoani humo na kuahidi kuhakikisha maelekezo yote ya Naibu Waziri Mkuu yanatekelezwa kwa wakati, ikiwemo ujenzi wa uzio wa shule na upatikanaji wa vifaa vya maabara huku Akiwasihi wazazi kupeleka watoto wao shule ili waweze kutumia fursa ya elimu na kufikia ndoto zao.
Awali Mkuu wa shule hiyo ,Ester Kobelo alieleza kuwa shule hiyo iliyopo kata ya rbomba katika kijiji cha Oltepes wilayani humo ilianzishwa mwaka 2024 ikiwa ni sehemu ya shule 26 za aina hiyo hapa nchini ,na hadi sasa ina wanafunzi 310 na utekelezaji wa awamu ya kwanza ya ujenzi wa vyumba vya madarasa jengo la utawala Maabara ya Fizikia na Geography na jengo la vyoo nk unaogharimu kiasi cha sh,bilioni 3 umekamilika.
Alizitaja baadhi ya changamoto ni pamoja na ujenzi wa ukuta ambao Dkt biteko aliitaka halmashauri ya wilaya ya Longido kuanza mchakato haraka wa ujenzi unaogharimu kiasi cha sh,milioni 730 ili kuepuka wanafunzi kuvamiwa na wanyama kutokana na eneo hilo kuwa na historia ya wanyama wakiwemo wakali.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Biteko alitembelea na kukagua mradi wa shule ya sekondari ya Longido Samia iliyopo Wilayani Longido ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku nne mkoani humo kuelekea maadhimisho ya miaka 61 ya Muungano wa Tnganyika na Zanzibar Aprilu 26 kila mwaka,ambapo kqa mwaka huu yataadhimishwa kila mkoa.
Mwisho.