Na Mwandishi wa A24tv.
KAMPUNI ya Vinywaji Vikali ya Mega Beverages Limited ya Jijini Arusha kupitia Chapa yake ya K- Vant Premium Spirit, imetunukiwa Medali ya fedha ya kinywaji bora (Best Spirit by Value) katika Mashindano ya London Spirits 2025 yaliyoshirikisha wazalishaji zaidi ya 500 duniani.
Kwa kupindi cha miaka 8, Shindano la London spirits limekuwa mojawapo ya mashindano ya kimataifa ya Spirits yanayoheshimika zaidi. Tofauti na mashindano ya kitamaduni ambayo huhukumu Spirits tu kwa ladha.
K- VANT IPER
K VANT G SPECIALEHTIN
Shindano la London Spirits hutuza Spirits kulingana na ubora, thamani, na ufungaji – mambo matatu muhimu yanayoathiri maamuzi ya ununuzi wa watumiaji.
Shindano la London Spirits hutuza Spirits kulingana na ubora, thamani, na ufungaji – mambo matatu muhimu yanayoathiri maamuzi ya ununuzi wa watumiaji.
Shindano la mwaka huu lilileta pamoja jopo la baadhi ya wanunuzi wa Spirits, Bartenders, Mixologists, Waagizaji, na wataalam wa sekta duniani kote.
Jamuzi huo ulifanyika London mnamo Machi 2025, ambapo zaidi ya washiriki 500 kutoka zaidi ya nchi 30 za wazalishaji wa pombe mashuhuri duniani walitathminiwa na kupata alama.
Kushinda tuzo mbili katika Shindano la London Spirits kunamaanisha kuwa K-Vant Premium Spirit ilichomoza kati ya makampuni ya kimataifa katika mojawapo ya vyumba vya kuonja ubora wa vinywaji.
“Miongoni mwa sifa za uthibitisho wa ubora na thamani ya juu ni pamoja na ufungaji wa kipekee wa chapa ya K-Vant Kama biashara.
inayomilikiwa na familia iliyoanzishwa na wajasiriamali shupavu, tunayo heshima ya kutambulika kimataifa” Alisema Chris Ndosi, Meneja Mkuu wa Mega Beverages Limited.
Mwisho.