Na Mwandishi wa A24tv Arusha .
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Paul Christian Makonda leo Mei 21,2025 amemuapisha Lameck Karanga Ng’ang’a kuwa Mkuu wa Wilaya ya Karatu ambapo uapisho umefanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo.
Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alimteua Lameck Ng’ang’a kuwa Mkuu wa Wilaya ya Karatu Mei 06,2025 akichukua nafasi ya Mhe. Dadi Horace Kolimba ambaye alihamishiwa kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga.
Kabla ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya, Ng’ang’a alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Karatu
Mwisho .