Na Mwandishi wa A24Tv
Halmashauri ya Arusha DC inatekeleza Mradi wa Ujenzi wa Madarasa 8 katika Shule mpya ya Sekondari ya kata ya Kiutu wilayani Arumeru.
Akiongea Wakati Mkurugenzi na viongozi wa Halmashauri hiyo walipotembelea kukagua shule hiyo Diwani wa kata ya Kiutu Malaki Malambo amesema wanaishukuru serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha za Utekelezaji wa miradi.
Amesema kwamba fedha iliyotengwa imetumika vizuri hakuna ubadhirifu na Mkurugenzi ameahidi kuongeza fedha kwa ajili ya kumalizia kazi iliyoanzwa na wananchi ambapo Kuna Madarasa nane hayajakamilika ili January wanafunzi waanze masomo kwa kidatocha kwanza.
Ameeleza kwamba serikali kupitia Halmashauri imejielekeza kuifanya shule hiyo kuwa na kidato. cha tano na cha kwanza ambayo itapokea hapo mwakani wanafunzi wa kidato Cha kwanza January.
Kwa Upande Wake Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Selemani Msumi ameahidi kutoa fedha za umaliziaji wa shule hiyo na kusema kuwa wapo katika Mchakato wa kusubiria fedha.
Amesema kwamba pamoja na Lengo shule hiyo imekuja wakati muafaka Halmashauri inapojiandaa na mkakati wa kuongeza vyanzo vya mapato na kumshukuru Diwani wa kata hiyo kwa kutoa eneo la ujenzi wa shule hiyo
Mkurugenzi huyo wa Halmashauri Anabainisha kwamba fedha za Mradi huo ni kiasi Cha Milion 470 ya fedha zilizotolewa na Mh. Rais Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya ujenzi wa sekondari hiyo mpya ya kata ya Kiutu ikiwa ni sehemu ya Utekelezaji wa sekta ya Elimu.
Airene Olais Mkazi wa Kijiji Cha Olgilai kata amesema wanaishukuru Halmashauri hiyo na viongozi kwa kuja na wazo la kuanzisha shule hiyo kwani awali kata hiyo haikuwa na shule hivyo imekuja Wakati muafaka
Amesema kwamba shule hiyo pia itawasaidia watoto wa Jamii ya kifugaji kutotembea umbali mrefu kwenda kata za jirani kufuata shule kwani Sasa itakuwa Karibu na kata hiyo.