Katika hatua nyingine waziri Biteko alisema kuwa serikali iko katika mpango madhubuti wa kujenga Kituo cha Tanzanite City kitakachojengwa katika Mji wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara lengo ni kutaka Madini hayo kuwanufaisha Wafanyabiashara na wachimbaji Wadogo Wadogo wa Madini ya Tanzanite.
Waziri Biteko alisema sekta ya Madini imepanda katika ukusanyaji kutoka asilimia tano hadi kufika asilimia Saba na kufanya uuzwaji wa Madini nje ya Nchi kuwa Mzuri na Wenye tija Kwa serikali.
Mwaka 2020 serikali ilimtangaza bilionea Saniniu Laizer aliyepata mawe yenye ukubwa wa zaidi ya kilogramu 7.8 na kufuatiwa pia na bilionea wa madini ya Ruby Sendeu Laizer akitokea wilaya ya Longido mkoani Arusha.