Na Mwandishi wa A24Tv .
Leo Oktoba 01, 2022 Mamia ya wananachi wa mkoa wa Geita na mikoa ya jirani wamemiminika kwenye Banda la Tume ya Madini katika Maonesho ya Tano ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika Viwanja Bombambili mjini Geita.
Elimu inatolewa katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na fursa za uwekezaji katika sekta ya madini, taratibu za upatikanaji wa leseni za madini nchini, biashara ya madini na taratibu za usalama wa afya na mazingira kwenye migodi ya madini.
Maeneo mengine ni pamoja na namna watanzania wanaweza kushiriki katika Sekta ya Madini kupitia utoaji wa huduma mbalimbali kwenye migodi ya madini na mchango wa kampuni za uchimbaji wa madini kwenye jamii.
Pia inatolewa huduma ya usajili wa leseni za madini kwa njia ya mtandao (Online Mining Cadastral Transactional Portal) na upimaji wa madini ya metali.