Na Doreen Aloyce, Dodoma
Tanzania ina Zaidi ya ndege zilizosajiliwa 400 ambazo zimekifanya chuo cha usafirishaji nchini NIT kuanzisha mafunzo ya urubani sanjari na kununua ndege mbili za mafunzo kutoka nchini Marekani zenye thamani ya dola milioni 1.2.
Akiongea na waandishi wa habari Jijini Dodoma Mkuu wa Chuo cha Usafirishaji nchini NIT Prof. Zakaria Mganilwa ameeleza kwamba asilimia 60 ya marubani nchini wanatoka nje ya nchi hivyo wameona ili kupunguza ombwe la upungufu wa marubani wazawa chuo hicho kimeanzisha mafunzo ya urubani.
Amesema Serikali imetenga fedha za kuanzisha kozi mahusisi kiasi cha billion 50 ikiwemo ujenzi wa majengo matano yenye thamani ya billion 21 pamoja na kuanzisha kozi ya mafunzo ya uhandisi wa reli ya uendeshaji wa reli ya mwendokasi ya SGR sanjari na wataalamu wa uhandisi wa meli.
Amesema kwamba serikali imetenga hekari 60 katika kiwanja cha ndege Kilimanjaro KIA kwa ajili ya chuo hicho cha marubani sanjari na mkoani lindi kwa ajli ya chuo cha Usafrishaji wa majini kwa ajili ya watengenezaji wa meli na uchomeaji ikiwa ni sehemu ya utekeleza wa uchumi wa bluu.
“Serikali ina miradi ya kimkakati inatekeleza kupitia chuo cha Usafirisshaji tunajenga majengo matano Mabibo kwa billion 21 na teyari tumeshasaini na mkandarasi pia tuna maeneo mengine yametengwa kwa ajili ya kuanzisha kozi mbalimbali zikiwemo za utengenezaji wa Meli Wataalamu wa utoaji wa huduma za Reli ya Mwendokasi SGR’’
Kwa mujibu wa Prof,Mganilwa amebainisha kwamba kwa sasa chuo hicho kinatoa Astashahada ya Uhandishi wa reli uhandisi wa ndege huku akisema serikali imewekeza kwenye SGR nao wamejipanga kutoa Rasilimali sahihi na kutumia fursa hizo kuanzisha kozi katika maeneo tofauti ya usafirishaji.
Kwa Upande wake Msemaji Mkuu wa Serikali Gelison Msigwa amesema kwamba Sekta ya usafirishaji nchini imeendelea kuboreshwa na chuo hicho kimeendelea kuboresha kozi mbalimbali kwa lengo la kutoa hduma bora kwa wananchi na kuzalisha wataalamu wenye weledi kwa maendeleo ya Taifa.
Hatahivyo Amesema serikali pia imetoa fedha kiasi cha billion 50 kwa lengo la kuhakikisha chuo hicho kinafikia malengo ya kuazalisha rasilimali watu zenye ubora utkaosaidia kuongeza kasi ya serikali kutoa huduma bora kwa wananchi,
Mwisho