Na Juliana Laizer
Mbunge wa Jimbo la Monduli mh Fredrick Lowassa ameelekeza mara Moja kufanyika kwa ukarabati wa madarasa matatu katika shule ya msingi Kilimatinde kata ya Moita , yenye uhitaji mkubwa wa sakafu na Kuta
Fredrick ametoa agizo Hilo katika mahafali ya tatu ya darasa la Saba katika shule hiyo ambapo amesema madarasa hayo atayakarabati mwenyewe na kumtaka Diwani na viongozi wengine wa serikali pamoja na kamati ya shule kumtafuta fundi Ili kuangalia na kupima Gharama ya ukarabati wa madarasa hayo Ili ukarabati huo uanze mara Moja ambapo wazazi nao walimshika mbunge mkono Kwa harambee iliyoendeshwa na Diwani wa kata hiyo mh Damuni huku nguvu ya jamii ikitakiwa katika ujenzi wa vyumba vya walimu
Aidha kwa upande mwingine Frederick ametoa computer pamoja na printer Kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi hao katika masomo ya TEHAMA.
” Lakini pia niseme kwamba Elimu ya msingi kipindi Cha nyuma ilionekana ni ya thamani sana na unaweza kuendelea na maisha mengine lakini Kwa Sasa Hii sio Elimu ya msingi mnatakiwa kuendelea mbele Hadi kidato cha sita, sanasana wadogo zangu au watoto wangu wa kike mliohitimu Leo msikatishwe malengo yenu Kwa kuozeshwa mkiwa Bado wadogo, wazazi tuwasomeshe watoto Hawa , tuwape Elimu tusiwabadilishe Kwa mifugo Kwani wakifanikiwa zaidi katika Elimu watawaletea ng’ombe zaidi .
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Moita Prosper Meyan Damuni Amemshukuru Mbunge Kwa kujitoa Kwa Khali na Mali kwa ajili ya watoto hao Kwa ukarabati wa madarasa matatu na kusema itakuwa chachu kwao kuchochea Elimu ,pamoja na kuwashukuru Wazazi wote walioonyesha Nia na madhumuni, na kuahidi ujenzi huo kuanza mara Moja pamoja utunzaji wa Miundombinu hiyo.
Awali wanafunzi wao wakati wakisoma Risala Kwa mgeni Rasmi wamesema pamoja na kukabiliana na changamoto mbalimbali , tatizo la Maji, uchakavu wa madarasa , upungufu wa Walimu pamoja na vifaa vya Tehema imekuwa changamoto kubwa kwao , ambapo mbunge huyo ambaye ndiye mgeni rasmi katika mahafali hayo ameahidi kukabiliana na kero hizo huku ukarabati ukianza mara Moja .