Na Geofrey Stephen Arusha
Nabii Mkuu wa Kanisa la Ngurumo ya Upako Geor Davie ametoa hundi ya sh,milioni 100 kwaajili ya kusaidia wafajasiamali wa soko la Samunge lililopo Kata ya Kati Jijini Arusha ili waweze kujionea kiuchumi.
Aidha amesena kuwa yeye sio mwanasiasa bali anamshukuru Mungu kwani baraka imekuja na kutoa rai kwa viongozi wa dini rudisheni sadaka walizotoa waumini wetu
Pia alishukuru wananchi waliobeba picha na mapokezi mazuri na kusema kuwa awali aliandaa hundi ya sh,milioni 50 lakini baada ya kuona umati huo na chagamoto za soko hilo ameongeza tena sh,milioni 50 nyingine.
Alisema sh,milioni 80 inaenda kwa watu wenye uhitaji wafanyabishara hao huku sh,milioni 20 zikiingia katika ukarabati huo wa soko hilo
Nabii huyo mkuu ambaye ni Balozi wa Amani alisema neno amani halina dini na aliomba wananchi wamuunge mkono Rais Dk,Samia Hassan Suluhu.
Alisema alipokea barua ya kuomba msaada katika soko hilo na alimshukuru Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini,Mrisho Gambo kwakutoa ahadi ya sh,milioni 10 katika soko hili.
Alishukuru kwakuwa mlezi wa soko hilo ingawa hata weza ulezi wa moja kwa moja na atashirikiana nao katika kila hitaji.
Alisema awali miaka ya nyuma aliamua kuleta injili kwa maneno na badae akabadilika akaanza kueneza injili kwa matendo (vitendo) na maneno machache sasa kazi kubwa zaidi.
Alisema anapoona vijana wanateseka mitaji,maisha magumu na kunakitu kimemshangaza katika maisha mama anamtaji wa sh,15000 lakini anajenga na kunawatu ukiwapa sh,50000 au sh,100000 anafika mbali.
Aliomba viongozi wa dini kurudisha sadaka kwa jamii kwani wamehubiri sana na kunawatu wanashida wanaotoa sh,500 na sh ,1000 hebu tureremke kwa jamii wanaotoa sadaka
“Huwezi kusaidia jamii kila mmoja tumsaidie Rais Samia kwa kusaidia jamii kwa kiasi fulani,mimi sio tajiri bali mungu ametuinua nami niwape wengibe”
“Msaada huu ninaotoa usibague watu bali kila mmoja apewe kwa kadri utakavyopewa nipo hapa kusaidia jamii na naomba niletewe majina ya hao wafanyabiashara niwaombee ”
Naye Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini,Mrisho Gambo akisalimia wananchi wa eneo hilo kabla ya nabii huyo kuongea na wafanyabiashara hao alisema wakati nabii huyo akiandaa ziara hiyo sokoni hapo kunamaneno maneno yaliibuka.
Awali wakati akisoma Chuo Cha Uhasibu Arusha(IAA) kunamama moja alimchukua akampeleka kwa nabii huyo kuombewa na leo hii amefika hapa.
Alisema kunawatu wanakereka sana Geordavie kuitwa Nabii Mkuu na yeye anamuita Nabii Mkuu kwasabababu anaheshimu kipawa alichopewa nabii huyo.
Alisema katika soko hilo kunamambo matatu yanayolikabili na mwaka 2019 soko hilo liliungua na hakukuwa na msaada wowote bali wajasiriamali hao waliishi kwa changamoto hizo kwa muda mrefu ikiwemo mitaji.
Alisema soko hilo linachangamoto za mitaro,majengo ikiwemo usumbufusumbufu wa migambo na waliposikia unakuja hapa kunabaadhi ya migambo walichukua vitu vya wafanyabiashara hao.
“Kunabaadhi ya mambo niliyafanya sokoni hapa ikiwemo kisima Cha maji na nilitoa sh,milioni 20 kwakinamama 100 kunawengine walirudisha na wengine waliweza kurudisha namuachia mungu”
Aliahidi kutoa sh,milioni 10 kwaajili ya ujenzi wa soko hilo na hakuna mtu atakayepewa hela mkononi lakini soko hili lipo chini ya halmashauri tutakaa vikao na madiwani wenzangu ili tubadilishe soko hili ili liwe la kisasa kwanibaadhi ya Wataalam wakipelekewa hoja ya soko hilo kubadilika wanapingapinga tu hivyo ukiwaombea watabadilika .
Alisema anatambua jinsi anavyokomboa watu mbalimbali,mitaji,fedha,pikipiki na hiyo ndio maana ya utumishi wa mungu kwani anachovuna ndicho anachokula na watumishi wake.
Pia alitoa salamu za Mkuu wa Wilaya ya Arusha,Said Mtanda na kusema DC yupo pamoja na yeye kwani anatambua kazi nzuri anazofanya
Gambo alitahadharisha fedha hizo ziwafikie wanyonge kwani zimeombewa hivyo walengwa wataotafutwa wawe ni watu wafanyabiashara wa soko hilo kwelikweli kwani hela hiyo inaupako iachiwe iguse maisha ya watu
Naye Diwani wa Kata ya Kati,Abdulrasul Tojo alimpongeza Nabii Geordavie kufika eneo hilo na madiwani hao waliomba kwa pamoja kurodhia soko la Samunge kuwa chini ya nabii huyo
Alisema soko hilo baada ya kuungua miaka mitatu iliyopita wafanyabiashara waliunguliwa bidhaa zao eneo hilo na hadi sasa halijajengwa
“Tunaomba ukiwezekana madiwani waridhie soko hili liwe chini yako kwani wajasiriamali hawa wanahitaji furaha na amani kutoka kwa watu mbalimbali hivyo madiwani naomba mridhie soko hil likiwa chini yako”
Naye mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Arusha,Ofisa Tarafa wa kata hiyo ,Chausiku Baha alisema yeye kama ofisa tarafa huyo atawasiliana na nabii huyo ili kuzitatua”
Naye mwakilishi wa Wafanyabiashara hao , ambaye ni katibu wa Afya Soko la Samunge , Loveless Joakim akisoma risala Alisema soko hilo lilianzishwa 12 ,Septemba mwaka 2012 likiwa na jumla ya vibanda 2106 likiwa na wafanyabiashara 2,106
Alisema wafanyabiashara hao wanajihusisha na uuzaji wa bidhaa mbalimbali na lipo chini ya halmashauri ya Jiji la Arusha na Machi 28 mwaka 2019 soko hilo liliungua na bidhaa ziliungua huku mitaji ikiungua.
Alisema soko hilo halina mageti ya kutosha na ujio wake nabii huyo utawezesha wafanyabiashara kujikwamua kiuchumi na kujipatia mahitaji yao.
Alishukuru Rais Dk, Samia Hassan Suluhu na viongozi mbalimbali kwakujali wafanyabiashara hao na kuwatakia afya njema viongozi hao
Awali kabla ya Nabii kufika eneo hilo la Samunge wajasiriamali wanaofanya biashara zao katika Soko la Samunge walimiminika kushuhudia ujio wa nabii huyo kwaajili ya wafanyabishara hao
Wafanyabiashara hao wakiwa na kanga ,wengine mabango mbalimbali wakimsifu Nabii huyo yaliyoandikwa Eeh Nabii Mkuu Sis Wanao,Vijana Tumjue Mungu,Maajabu ya Nabii Mkuu Karne ya 21 Watapita Wapi”
Hata hivyo barabara ya Samunge ilikuwa na msongamano mkubwa wa magari baada ya watu wengi kujitokeza na wengine wakicheza barabarani na baadae ilifungwa kabisa.
Huku hekaheka na amsha amsha za salamu mbalimbali kutoka kwa watumishi wa nabii huyo wakiongozwa na Esther jina maarufu la mama Alphard na Baba Alphard ambaye ni Nabii Daudi Mashimo waliopewa magari na kuongeza kuwa hakuna maskini katika eneo hilo
Mashmo alisema alipewa gari na fedha hivyo siyo ndoto kila mtu anaenda kupokea fedha sawasawa na wengine.
“Nabii Mkuu ni baba ni yetu leo ameonekana hapa, hivyo mtapokea fedha hapa ili biashara zenu zineemeke”.
Mwisho