Na Richard Mrusha
Mkurugenzi wa mgodi wa Igalula na shabiki wa kilabu ya Yanga Bwana Husein Makubi (Mwananyanzala ) amejitokeza hadharani na kusema yuko tayari kumsapoti Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania dkt Samia Suluhu Hassan. kwa kutoa kiasi cha fedha taslimu shilingi laki tano kwa kila goli kwenye vilabu viwili yanga na simba vinavyoshiriki kwenye michuano ambapo simba inashiriki ligi ya mabingwa Afrika na Yanga inashiriki michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika.
Mwananyanzara amesema amefanya hivyo ili kuwapa hamasa vijana piandi wawapo uwanjani wajitume kwa bidii ili waweze kuleta ushindi
Nimeamua kumunga mkono Rais kwa kuwa anamambo mengi ya kufanya sisi ambao tupo na tunapata mda kama hivi ni vyema kujitoa kwa ajili ya vilabu vyetu ili viendelee kufanya vizuri maana ushindi wao ni ushahidi wetu sote kama taifa ndugu mwandishi wa habari mimi ni shabiki wa Yanga kindaki ndaki ila nimeona nisapoti na kilabu ya simba kwa vile ni watani zangu”, amesema mwananyanzara.
Ameongeza kuwa nategemea kuelekea jiji Dar es laam wiki ijayo ambapo nitakabidhi shilingi laki tano kwa kilabu ya simba tarehe 16,3,2023 kwa vile ilishinda goli moja ambalo lilifungwa na Clatous Chama kati ya mechi ya simba na Vipers
Pia,17,3,2023atakabidhi shilingi milioni moja kwenye kilabu ya Yanga ambayo ilishinda magoli mawili ambayo yalifungwa na Wachezaji wawili la kwanza Fiston Mayele na la pili likafungwa na Jesus Moloko ambapo Yanga ilicheza na timu ya Real Bamako.
Ameongeza kuwa ameishaongea na uongozi wa timu zote mbili kwa maana ya simba na Yanga hivyo wameshakubaliana namna ya kuja kukabidhi kiasi cha hizo fedha alizoahidi.
Ameongeza kuwa ataendelea kutoa fedha kwa mechi zingine zitazoendelea kuchezwa.