Author: Geofrey Stephen

Matukio ya uhalifu ,ubakaji na wizi yazidi kutikisa kata ya Daraja mbili mkoani Arusha . Na Geofrey Stephen Arusha . Matukio ya uhalifu katika kata ya Daraja Mbili Mkoani Arusha yamezidi kushika kasi mara baada ya Mtendaji wa kata hiyo John Joseph kunusurika kuchomwa kisu cha ubavuni na kibaka wakati akiwa katika harakati za kumwokoa msichana aliyetambulika kwa jina la Caren Nyangasa (20) aliyenusurika kufanyiwa kitendo cha ubakaji na kibaka aliyetambulika kwa jina la Bolo young . Akizungumzia tukio hilo,Mtendaji wa kata hiyo amesema toka mei mwaka huu hadi sasa hivi kata yake imekuwa na matukio makubwa ya uvunjifu wa…

Read More

Na Mwandishi wa A24Tv Arusha .  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Posta Afrika (PAPU) Dkt. Sifundo Moyo wakati wakivuta kamba kuashiria ufunguzi wa Jengo la Makao Makuu ya Umoja wa Posta Afrika (PAPU Tower) lililopo eneo la Philips Jijini Arusha tarehe 02 Septemba, 2023. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Posta Afrika (PAPU) Dkt. Sifundo Moyo, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye pamoja na viongozi wengine wakati akikata utepe kuashiria…

Read More

Arusha Na Mwandishi wa A24Tv . Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imewahukumu aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Dk. John Marco Pima na wenzake wawili kifungo cha kwenda jela miaka ishirini baada ya kukutwa na hatia kwa makosa tisa ya uhujumu Uchumi ikiwemo la utakatishaji fedha. Hukumu hiyo imetolewa leo Alhamisi Agosti 31, 2023 na Mhe. Hakimu Serafina Nsana kwa shauri namba 05/2023 la uhujumu uchumi, lililokuwa likiwakabili Dk. Pima na wenzake Bi Mariam Mshana aliyekuwa Mweka Hazina wa Halmashauri ya Jiji la Arusha na Bw. Innocent Gitubabu Maduhu, aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji…

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha . Chama cha wafanyabiashara wenye viwanda na kilimo TCCIA, kimetoa  mafunzo ya uhusishwaji wa kibiashara kwa wamachinga,vijana, wamama wa sokoni na watu wenye ulemavu. Akifungua mafunzo hayo Mstahiki Meya wa jiji la Arusha Maxmilliane Iranghe, amesema jiji la Arusha litatoa mikopo isiyokuwa na riba na riba nafuu kwa akina mama, vijana na watu wenye ulemavu” Amesema Jiji la Arusha Tumetenga takribani shilingi Billioni 4, Ela hii ikienda kwenye mzunguko itawatoa wafanyabiashara mahali walipo kwenda sehemu wanapotaka kufanya biahara . Mstahiki Meya amehasa makapuni mengi kuendelea kuandaa mafunzo kwa wajasiriamali kwa kuwapatia elimu itakayowainua kibiashara ilikuendelea kutengeneza…

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha . Naibu Katibu Mkuu wizara ya Mifugo,Dokta Daniel Mushi ameutaka uongozi wa wilaya ya Longido kujipanga na kuweka doria za kutosha mipakani ili kuzuia utoroshaji wa mifugo ambayo inapelekwa nchi jirani ya Kenya na kupelekea kuwepo kwa upungufu wa mifugo nchini. Ameyasema hayo leo agosti 30 ,jijini Arusha akiwa katika ziara yake ambapo ametembelea mnada wa Mifugo katika eneo la Meserani pamoja na kiwanda cha kuchakata nyama cha Elia food Overseas kilichopo wilayani Longido mkoani Arusha. . Dk Mushi amesema , kumekuwepo na uhaba mkubwa wa Mifugo hapa nchini hivi sasa changamoto inayopelekea kushuka kwa soko…

Read More