Author: Geofrey Stephen

 Na Pendo Mkonyi, Arusha. Shule ya sekondari  Mwandeti ya mkoani arusha imeendelea kuwa kinara  kutokana na matokeo yake mazuri kufuatia mwaka huu  wa 2023 tena  katika matokeo ya kidato Cha 6 kufaulisha Kwa daraja la kwanza watahiniwa wote 77. Akizungumza  mara baada ya kutangazwa Kwa matokeo ya kidato Cha 6 nchini mkuu wa shule ya sekondari Mwandeti John Silvano Masawe amesema kuwa wanafunzi wote 77 waliofanya mitihani Yao ya kidato Cha 6 wamefaulu Kwa kiwango Cha juu na hawezi kulinganishwa na shule ya sekondari Ilboru na kisimiri Pichani: ni mkuu wa shule ya sekondari Mwandeti John Silvano Masawe. Masawe amesema…

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha . Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Nape Nnauye amezindua programu ya Shahada ya Media Anuwai na Mawasiliano kwa Umma katika chuo cha uhasibu Arusha-Kampasi ya Arusha . Akizindua kozi hiyo Nape amesema kuwa,kitendo cha kuzinduliwa kwa programu mpya chuoni hapo ni jambo kubwa sana  kwa maslahi ya nchi na linapaswa  kuigwa  na vyuo vingine ili kuweza kupata wataalamu wengi zaidi waliobobea katika fani hiyo. Nape amesema kuwa,kuwepo kwa programu hiyo katika chuo hicho kutasaidia kupata wataalamu bora na wa kipekee  waliobobea na kuondokana na changamoto  ya kuwa na wanataaluma  katika fani  hiyo ambao hawajabobea …

Read More

Na Doreen Aloyce, Dodoma Serikali ya Kanada imetoa kiasi cha Shilingi Bilioni 240 kwenye Mfuko wa Afya ya pamoja (Health Basket Fund) ili kusaidia Sekta ya Afya nchini. Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amebainisha hayo leo Julai 20, wakati wa mkutano wa utekelezaji wa shughuli za Mfuko wa Afya wa Pamoja (Health Busket Fund) HBF na Waziri wa Maendeleo ya jamii Kanada Jijini Dodoma. “Tunaishuku sana Serikali ya Kanada kupitia Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Kanada Mhe. Harjit Sajjan kwa kusaidia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kiasi cha shilingi Bilioni 240 kwa ajili ya kuboresha sekta…

Read More

Magonjwa yasiyoambukiza huchangia asilimia 33 ya vifo nchini. Na. Catherine Sungura, Dodoma Magonjwa Yasiyoambukiza (NCDs) yanachangia takribani 33% ya vifo vyote nchini huku kwa takwimu za Shirika la Afya duniani (WHO) kwa mwaka 2020 zinaonesha kuwa magonjwa hayo yalichangia zaidi ya vifo milioni 41 sawa na 71% ya vifo vyote Duniani ukilinganisha na vifo milioni 57 kwa mwaka 2016 duniani. Hayo yameelezwa leo na Waziri wa Afya kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Ally Mazrui wakati wa Uzinduzi wa Utafiti wa Kitaifa wa Viashiria vya Magonjwa Yasiyoambukiza (STEPS SURVEY 2023) uliofanyika kwenye ukumbi wa Tawimu Jijini Dodoma. Mhe. Mazrui amesema…

Read More

Na Geofrey Stephen Karatu. Paroko wa Kanisa la Katoliki Parokia ya Karatu Jimbo la Mbulu, Mkoani Arusha Pamphili Nada ameuwa kwa kupigwa na chuma ya mlango wa kanisa mara baada ya kuingia Kanisani kwa nguvu kutaka kusali kufanyiwa maungamo baada ya kusema ameteseka kwa muda mrefu na mapepo. Mara baada ya kuingia kanisani  kichaa huyo aliyejulikana kwa jina la Romani Leonard (30) kufanya mauwaji hayo nae akauawa na Wananchi wenye hasira kali baada ya kengele kulia ya kanisa na waumini kufurika katika kanisa kujua nini kimetokea kanisani hapo . Waumini wa parokia hiyo mara baada ya kufika kanisani hapo walikuta…

Read More

Arusha na Geofrey Stephen Katibu Mkuu Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mohamed Hamis akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari juu ya Namba maalumu ya Utambuzi kwaajili ya utoaji huduma.  Mkurugenzi wa TEHAMA Priscus P. Kiwango akitoa ufafanuzi juu ya Namba Jamii kwaajili ya utambuzi wa utoaji huduma kwa mwananchi Kikao cha kujadili uanzishaji wa namba maalumu kwaajili ya utambuzi kwaajili ya utoaji huduma za serikali kati ya Katibu Mkuu Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mohamed Hamis Kilichofanyika Jijini Arusha katika hoteli ya Mountmeru.  Kikao cha kujadili uanzishaji wa Namba maalum kwaajili ya utambuzi kwaajili ya utiaji huduma za serikali kiikiendelea…

Read More

Na Doreen Aloyce, Dodoma Mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA imetoa wito kwa jamii kuwa na kumbukumbu na watu ambao waliwasajilia laini za simu kwa kutumia kitambulisha cha Nida maana wanaofanya utapeli ni watu wao wa karibu .. Hayo yameelezwa Jijini Dodoma na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dkt. Jabir Bakari alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA na maendeleo ya Mawasiliano. “Niwasihi watanzania kuweni makini na matapeli kila siku watu wanalia kuibiwa wanapigiwa simu na watu wao wa karibu na matokoeo yake wanatapeliwa”alisema Bakari. Aidha Mamlaka hiyo imesema kuwa Utoaji wa huduma…

Read More