Author: Geofrey Stephen

Na Mwandishi wa A24Tv Arusha . Kesi ya madai ya sh,milioni 123 inayoikabili kampuni ya Mabasi ya Kilimanjaro Track co.ltd dhidi ya Msanii wa kizaźi kipya,Nuni Suleiman(35) Mkazi wa Dar es salaam, imeunguruma katika mahakama ya wilaya Arusha. Shahidi wa kwanza katika shauri hilo la Madai namba 36 la mwaka 2022,  Nuni Suleimani,mbele ya Hakimu Mwandamizi Wilaya ya Arusha,Bitony  Mwakisu ,amedai  mahakamani hapo kuwa kampuni hiyo ya Kilimanjaro imejinufaisha kwa kutumia nyimbo yake ya Tabasamu Tanzania kujitangaza kibiashara kupitia mitandao ya kijamii bila idhini yake na kudai fidia ya kiasi hicho cha fedha. Alidai hayo wakati akiongozwa na wakili wake,Lillian…

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha RAIS Samia Suluhu Hassan,Augosti 19 anatarajiwa kufungua kikao kazi cha Wenyeviti na Wakurugenzi wa mashirika ya umma na Taasisi za Serikali,utakaofanyika katika  Ukumbi wa mikutano ya kimataifa,AICC Jijini Arusha. Mkuu wa Mkoa wa Arusha,John Mongela,ameyasema hayo  Augosti 18 alipokuwa akitoa taarifa ya maandalizi ya kikao hicho kwa vyombo vya habari na  kusema mbali na Rais,Viongozi wengine watakaokuwepo ni pamoja na Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa,Spika wa Bunge,Dkt Tulia Acksoni na mawaziri wa wizara mbali mbali . Ameongeza kuwa Augosti 21, Rais Samia,atakuwa mgeni rasmi kwenye madhimisho ya miaka 60 ya Kanisa la Kiinjili la kiluthelu Nchini,KKKT yatakayofanyika kwenye…

Read More

Na Geofrey Stepgen Arusha . Mamlaka ya udhibiti usafiri Ardhini LATRA mkoani Arusha, imetangaza kumalizika kwa mgomo wa daladala uliodumunkwa takribani siku mbili katika jiji la Arusha  na kusababisha adha kubwa kwa wananchi, wafanyabiashara na wanafunzi. Aidha mamlaka hiyo imepiga marufuku kwa chombo cha usafiri cha Bajaj  kufanyabiashara ya kupakia abiria kama daladala badala yake imewataka kufanyabiashara hiyo kwa kukodishwa  na sio kwenda wakiokota abiria. Akiongea na vyombo vya habari afisa mfawidhi Latra mkoa wa Arusha, Joseph  Michael,  amewahakikishia wananchi kuwa  hakuna mgogoro wowote kwa sasa baina ya daladala na bajaj na tayari vituo vipya 50 vya daladala  vimepangwa kutumika…

Read More

Na Doreen Aloyce , Dodoma Viongozi wa taasisi mbalimbali za umma wameeleza faida za kubadilishana taarifa kidijitali kupitia Mfumo wa pamoja wa ubadilishanaji taarifa serikalini ujulikanao kama ‘Government Enterp9rises Service Bus’ (GovESB). Wakizungumza na mwandishi wetu katika nyakati tofauti, viongozi hao wameeleza kuwa, mfumo wa GoVESB umekuwa na faida nyingi ikiwemo kuongeza ufanisi wa utendaji kazi, kuokoa muda pamoja na gharama za uendeshaji wa taasisi. Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel, alisema Mahakama inabadilishana taarifa na taasisi mbalimbali ikiwemo Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Wakala wa Usajili wa Biashara…

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha Wagonjwa wapatao 35 kati ya 200 waliojiandikisha , wamefanyiwa upasuaji wa Nyonga na magoti bure katika hospitali ya Arusha Lutheran Medical Centre ALMC, kupitia mpango wa mama Samia Love unaotekelezwa  na madaktari bingwa kutoka Marekani kwa kushirikiana na madaktari wa ndani. Akiongea na vyombo vya Habari Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa hospital ya Arusha Lutheran Medical Center ALMC Godwel Kivuyo alisema kuwa wimbi la uhitaji wa huduma ya upasuaji kwa wagonjwa bado ni kubwa na katika awamu hii ya kwanza watafanya upasuaji kwa wagonjwa 50 na kati yao 35 tayari wameshafanyiwa upasuaji tangia kuanza kwa zoezi hilo…

Read More

Na. Mwandishi Wetu SERIKALI imeendelea kutoa kipaumbele katika kuendeleza sekta ya kilimo nchini kwa kuzingatia umuhimu na tija ya sekta hiyo katika maendeleo ya Taifa. Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi Agosti 15, 2023 wakati akihutubia katika kikao cha Awali cha Wadau kwa ajili ya zoezi la Tathmini ya Nusu Muhula na Uandaaji Mpango wa Utekelezaji wa Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDFP II) kwa miaka mingine mitano kilichofanyika Jijini Dar es salaam. Dkt. Yonazi amesema kuwa sekta ya kilimo ni muhimu…

Read More

Na Geofrey Stephen Kia kilimanjaro Jombo la Madaktari Bingwa kutoka Marekani wametua leo katika uwanja wa kimataifa wa kia tayari kuelekea Jijini Arusha kutoa huduma ya upasuaji wa nyonga na magoti . Madaktari hao  60 bingwa wa upasuaji wa Nyonga na magoti kutoka nchini Marekani wamewasili nchini Kwa ajili ya upasuaji huo Kwa wagonjwa kutoka katika  maeneo mbalimbali nchini katika hospital ya Arusha Lutheran Medical Center ALMC Mkoani Arusha. Aidha Madaktari hao ambao wataanza upasuaji Kwa wagonjwa zaidi ya 200 kuanzia Tarehe 11 hadi 17 ya mwezi huu kwenye hospital ya Arusha Lutheran Medical Center iliyopo Jijini Arusha Akizungumza Mara…

Read More

Na Geofrey Stephen A24Tv Sakata la uvamizi haramu wa Mgodi wa Kitalu C wa Madini ya Tanzanite uliopo katika Mji wa Mirerani wilayani Simanjiro Mkoani Manyara unaomilikiwa na serikali na mbia mwekezaji mzawa kampuni ya kampuni ya Franone sasa imekuwa shamba la bibi­­­ baada ya wafanyabiashara wakubwa watatu kuingia katika mgodi huo na kuvuna madini ya mamilioni ya fedha bila hatua yoyote kuchukuliwa. Kampuni tatu zinazodaiwa kuingia Kitalu C na kuchimba kwa njia haramu maarufu kwa njia ya Bomu ni pamoja na kampuni ya Tanzanite  Explore inayomilikiwa na Victor Philipo Mkenga na Kampuni ya Saniniu Mining inayomilikiwa na Bilionea Saniniu Laizer  na…

Read More