Author: Geofrey Stephen

Mwandishi wa A24Tv Babati. Taasisi ya chemchem association ambayo imewekeza katika shughuli za Utalii katika eneo la Jumuiya ya hifadhi ya wanyamapori ya Burunge imetoa vifaa vya michezo kwa timu za wanawake na vijana katika vijiji 10 vinavyounda Jumuiya hiyo Lengo la kutoa vifaa hivyo ni kushirikisha wanawake na vijana katika uhifadhi kupitia michezo ambayo imeanza katika vijiji hivyo. Msimamizi wa miradi ya Jamii ya Taasisi hiyo,Nganashe Lukumay akizungumza katika Bonanza la timu za wanawake wa Kijiji Cha Mwada amesema vifaa hivyo vinatarajiwa kuziwezesha timu za wanawake na vijana kujiandaa na michuano ya Kila mwaka ya chem chem CUP. Nganashe…

Read More

*DKT. BITEKO ATOA SIKU 14 KUANZA UZALISHA WA ALMASI MWADUI* *Ujenzi wa Bwawa la Tope Laini wafikia asilimia 97* Mgodi wa Uchimbaji Mkubwa wa Madini ya Almasi wa Mwadui kuanza uzalishaji baada ya kusitisha uzalishaji kufuatia ajali ya kubomoka kwa bwawa la tope laini iliyotokea Novemba 07, 2022. Hayo ameyabainisha na Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko baada ya kutembelea Mgodi wa Williamson Diamonds Limited unao milikiwa kwa ubia kati ya Serikali kwa asilimia 25 na Kampuni ya Petra kwa asilimia 75. Dkt. Biteko ametembelea mgodi huo kwa lengo la kufanya ukaguzi wa ujenzi wa bwawa la kuhifadhia tope laini…

Read More

Na Richard Mrusha Tabora MKURUGENZI wa Biashara wa Asasi ya kusaidia sekta ya kilimo nchini (PASS TRUST) Adam Kamanda Amesema kuwa asasi hiyo inatoa dhamana kwa wakulima katika nyanja zote zinazoshughulika na kilimo cha mazao mbalimbali. Amesema kuwa PASS TRUST imeanzishwa na Serikali ya Tanzania Kwa kushirikiana na nchi ya Denmark kwa lengo la kuondoa changamoto ya Wakulima hasa wadogo ambao hawana dhamana ya sheria ya fedha kama inavyohitaji ambapo sheria ya nchi inahitaji mtu yeyote anayechukua mkopo aweze kuwa na dhamana walau asilimia 25. Mkurugenzi wa biashara wa asasi ya kusaidia sekta ya kilimo nchini Tanzania (PASS TRUST) Adam…

Read More

Na Mwandishi wa A24Tv. Siku chache baada ya kufunguliwa kwa mgodi wa dhaabu ulioko kijiji cha kilimamzinga kata ya Kang’ata Wilayani Handeni Mkoani Tanga unao milikiwa na mwekezaji mzawa Godfrey  Bitesigirwe  umeanza kazi za uzalishaji kama hapo awali kabla ya kufungwa. Mwekezaji wa mgodi wa Dhahabu Godfrey  Bitesigirwe akizungumza na vyombo vya habari kuhusu shughuli zikiendelea katika mgodi wake  Taarifa zilizo fanywa  na Kituo hiki  zimebaini  kwamba mara baada ya maelekezo ya Mh Naibu Waziri shughuli mbali mbali za uzalishaji za  uchimbaji wa dhaabu unaendelea pamoja na maboresho ya kuweka mazingira vizuri ikiwemo upandaji wa miti pamoja na kuondoa vibanda…

Read More

Na Gofrey Stephen Arusha . Prof Joyce Ndalichako, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu ameonya baadhi ya maofisa kazi nchini wanaotumia lugha za vitisho kwa waajiri na kutumia vibaya majina ya viongozi pindi wanapoenda kufanya kaguzi sehemu za kazi. Akizungumza jijini Arusha Waziri huyo akifungua mafunzo ya maofisa kazi kutoka mikoa yote 26 hapa nchini, yaliyoandaliwa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na masuala ya Ukimwi (UNAIDS), yenye lengo la kutoa mafunzo  ya ukaguzi sehemu za kazi kuhusu virusi vya Ukimwi na usalama kazini…

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha . SERIKALI ya watu wa China imetoa Msaada wa magari 8 yenye thamani dola 400,000 pamoja na vipuri vyake kwa jumuiya ya Afrika Mashariki( EAC) . Aidha pamoja nakuleta wataalamu wa kutoa mafunzo ya matumizi ya magari hayo kwa madereva na mafundi wa Jumuiya ya nchi za Afrika mashariki kwa ajili ya kuboresha shughuli za EAC. Akiongea mara baada ya kukabidhi magari hayo Balozi wa China nchini Tanzania CHEN MINJUAN kwenye makao makuu ya EAC Jijini Arusha amesema kwamba zoezi hilo lilikuwa lifanyike mwaka 2021 lakini kutokana na janga la uviko ndio maana limefanyika mwaka huu.…

Read More