Author: Geofrey Stephen

Na Geofrey Stephen Arusha Madaktari Bingwa wapatao 60 wa Mifupa na Nyongo kutoka Los Angelos Jimbo la Califonia Nchini Marekani wanatarajia kutua  Nchini Agosti 10 mwaka huu kwa ajili ya kutoa huduma ya matibabu bure ya upasuaji wa magoti na nyonga.   Madaktari hao  ambao ni marafiki wa Rais Samia Suluhu Assan watawasili nchini siku hiyo katika uwanja wa ndege majira ya saa 2 usiku na watafanya shughuli za upasuaji kwa wagonjwa 200 ambao tayari wameshajiandikisha  na shughuli hiyo wataifanya kwa wiki mbili katika hospital ya rufaa ya Arusha Lutheran Medical Centre ALMC, (Seliani) inayomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kiluthei…

Read More

Na Richard Mrusha MBEYA Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar Mhe. Shamata Shaame Khamis amehimiza wananchi kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali katika Mapambano Dhidi ya Virusi vya UKIMWI nchini kwa kuendelea kuzingatia elimu inayotolewa kuhusu masuala hayo. Ametoa rai hiyo Agosti 6, 2023 alipotembelea Banda la Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu katika maonesho ya Kilimo Kimataifa yanayoendeleo Jijini Mbeya. Maonesho ya mwaka huu yamebebwa na Kauli mbiu inayosema “Vijana na Wanawake ni Msingi Imara wa mifumo Endelevu ya Chakula” “Tunapaswa kuungana kwa pamoja, katika mapambano haya ya Virusi vya UKIMWI na kuhakikisha kila anayegundulika…

Read More

Na Mwandishi wa A24Tv .Mbeya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amekutana na Balozi wa Japan nchini Tanzania Balozi Yasushi Misawa kujadiliana kuhusu ushirikiano katika sekta ya elimu ikiwemo uendelezaji mafunzo Vyuo vya Ufundi ambapo kwa sasa inapewa msukumo mkubwa ili kuwawezesha vijana kupata Ujuzi. Majadiliano hayo yamefanyika leo Agosti 7, 2023 Mkoani Mbeya, ambapo pia wamezungumzia umuhimu wa kuongeza fursa za ufadhili wa masomo kwa Watanzania katika Elimu ya Juu nchini Japan. Balozi Yasushi ameeleza kwamba takribani Watanzania 40 kila mwaka wanapata nafasi ya kwenda kusoma nchini Japan kupitia Skolashipu ya African Business Education (ABE). Ameongeza…

Read More

Na Mwandishi wa A24Tv Kilimanjaro . Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt Ashatu Kijaji (Mb.) awataka Maafisa Biashara wote nchini kukagua bei ya Sukari duka kwa duka na atakae kutwa na bei zaidi ya shilingi 3,200 achukuliwe hatua za kisheria. Waziri Kijaji ameyasema hayo Agosti 2, 2023 alipotembelea Kiwanda cha kuzalisha Sukari cha TPC Mkoani Kilimanjaro kujionea shughuli za uzalishaji na kisikiliza changamoto walizonazo. Dkt. Kijaji amesema ni jukumu la Maafisa Biashara kutambua mfanyabiashara yeyote atakayeuza sukari juu ya bei kati ya 2800 na 3200 kumchukulia hatua. Dkt. Kijaji amesisitiza kiwa ni jukumu la Serikali kulinda bidhaa yoyote inayotengenezwa…

Read More

Na John Mhala,Longido Zaidi ya shilingi milioni 30 zimechangwa na Shirika la Mipango na Maendeleo ya Jamii Longido {CBO} na Shirika Mwenza la Nchini Marekani la Friends For African Development {FAD} kwa kushirikiana na wananchi na Mbunge wa Jimbo la Longido Mkoani Arusha,Dkt Steven Kiruswa Katika kuhakikisha mtoto wa kike wa jamii ya kifugaji anapata elimu ya uhakika na huduma kadhaa za kijamii. Hayo yalisemwa na  Dkt Kiruswa katika Kitongoji cha Kaale, kijiji cha Iloirienito kata ya Iloirienito Wilayani humo mara baada ya kushiriki tukio la nguvu kazi na wananchi baada ya kuona juhudi  za wananchi katika kuisaidia serikali ujenzi…

Read More

Na John Mhala,Longido Bibi Monica Nduyai{100} Mzaliwa wa Kijiji cha Idendui Wilaya ya Ngorongoro Mkoani Arusha amesherekea siku yake ya kuzaliwa{Happy Barthday} kwa kutimiza miaka mia moja{Karne Moja} kwa kugawa msaada wa Mahindi tani 20 kwa watu wenye kuishi katika mazingira magumu {masikini} katika kata zote zilizopo katika wilaya ya Longido Mkoani Arusha. Nduyai ambaye ni mama mzazi wa Mbunge wa Jimbo la Longido na Naibu Waziri wa Madini,Dkt Stephen Kiruswa alisherehekea siku hiyo nyumbani kwake katika Kijiji cha Ngosuak kata ya Engarenaibor Wilayani Longido sherehe ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi{CCM} na Jumuiya zake ngazi ya wilaya…

Read More

Na Mwandishi wa A24Tv .TANGA – Waumini wa dini ya Kiislamu kote  dunuani  wameaswa kujenga mazoea ya kusoma na kuchambua matukio ya tareekh ili kuweza kujua historia ya Dini yao ya vizazi  vyake. Hayo yameelezwa leo Mkoani Tanga na Mudir wa Muasas Sheikh Shaffi Muhammed Nina wakati wa maandamano ya Maombolezi ya kumbukumbu ya kifo cha mjukuu wa Mtume Muhamad ( S.A.W ) Imam Hussein ( A.S) aliyefariki mwaka wa sitini na moja Hijiria. Sheikh Shaffi amesema  kuna haja ya kusoma na kuchambua tareekh kwa kuwa vitabu vya mwenyezi Mungu vilikuja  vikiwa salama lakini kulingana na siasa za…

Read More