Author: Geofrey Stephen

Na Richard Mrusha kahama MKURUGENZI wa Manispaa ya Kahama ,Mkoani shinyanga Anderson Msumba amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Kwa kuendelea kumwamini na kumuacha aendelee kuiwakilisha vyema Serikali Kwa kuwatumikia wananchi wa Manispaa hiyo. Amesema anamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan Kwa kumuamini na kuendelea kumuacha kwenye kituo chake cha Kahama ili aiendelee kumuwakilisha kuendelea kuwatumikia wananchi Kwa kutatua kero mbalimbali ndani ya Manispaa hiyo. Msumba ameyasema hayo wilayani humo Juni 14 ofisni kwake katika mahojiano maalumu na waandishi wa Habari juu ya maendeleo ya Manispaa hiyo ambapo Amesema kuwa ataendelea kufanya kazi Kwa weredi ili kuweza kusonga mbele katika kuwaletea…

Read More

Mwenge wa Uhuru kitaifa na matukio mbali mbali Wilayani Lushoto Mkoani Tanga ulivyo zunguka na kuzindua miradi mbali mbali na wananchi kupata Fursa ya kupiga nalo picha sio wakubwa tu na mpaka watoto wadogo wabeba mwenge wa uhuru Mtoto ambaye ajafahamika Majina yake akiwa katika kati ya watumishi wa halmashauri ya Lushoto wakati wa kupokea Mwenge wa Uhuru kitaifa wilayani lushoto akiwa amebeba mwenge wa uhuru  Masista wa St Mary’s Mazinde Juu secondary Lushoto, shule bora kitaifa ya wasichana Lushoto Wakipokea mwenge wa uhuru

Read More

Na Geofrey Stephen Lushoto Tanga Matukio katika picha likionyesha uzinduzi wa daraja la kisasa la mlesa  kata ya Dule M wilayani lushoto ambapo Mwenge wa Uhuru Kitaifa ulizindua mradi huo mkubwa wa garama ya shilingi Milioni 270,892 ,140.00 fedha zinazotokana na tozo ya mafuta . Mradio huu umeanza kutekelezwa mnamo tarehe 02 mwezi wa 11,2022 ambapo ulitarajiwa kukamilika ambapo  kwa sasa mradi upo kwenye kipindi mtazamio . Aidha katika utekelezaji wa  mradi huo makundi mbali mbali ya wananchi walipata fursa ya kunufaika kwa kupata ajira za muda pia mradi baada ya kukamilika umefanikisha kuondoa adha ya usafirishaji iliyo dumu kwa…

Read More

Na Doreen Aloyce, Dodoma Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene, ameipongeza Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) kwa jitihada kubwa inazozifanya katika kukuza na kuimarisha Serikali Mtandao nchini. Simbachawene ameitoa pongezi hizo jana, alipofanya ziara ya kikazi katika Ofisi za Mamlaka ya Serikali Mtandao zilizopo Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma, kwa lengo la kukagua utekelezaji wa majukumu ya e-GA katika usimamizi wa matumizi ya TEHAMA kwenye taasisi za umma. Amesema kuwa, kuimarika kwa matumizi ya TEHAMA katika taasisi za umma, kunatokana na usimamizi mzuri wa e-GA katika kuimarisha jitihada…

Read More

Na Geofrey Stephen Lushoto . Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa,Abdalah Shaib Kaim,ametaka mradi wa Zahanati unaojengwa kwa gharama ya sh,mil 100.9 katika kijiji cha Kwemakame,wilayani Lushoto ,Mkoani Tanga,  kukamilika kwa wakati ili kusaidia huduma ya Afya kwa wananchi wanaotembea umbali mrefu wa zaidi ya km 25 kufuata huduma hiyo. Akiongea wakati mbio za mwenge wa Uhuru zilipotembelea Zahanati hiyo na kuweka jiwe la msingi,Kaim alimshukuru rais Samia suluhu Hassan kwa kuwezesha mradi huo na kutoa rai kwa wasimamizi wa mradi kuhakikisha unakamilika kwa wakati ili kuwapunguzia wananchi adha ya huduma ya afya . “Serikali imekuwa ikitoa fedha…

Read More

Na Doreen Aloyce, Dodoma Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) inalenga kuimarisha zaidi uhusiano wake na Chuo Kikuu cha Mzumbe kupitia mkataba wa makubaliano (MOU) unaotarajiwa kufanyiwa maboresho hivi karibuni. Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa e-GA Eng. Benedict Ndomba, wakati wa kikao cha Pamoja kati ya e-GA na Chuo Kikuu cha Mzumbe kilichofanyika leo katika ofisi za e-GA jijini Dodoma, kwa ajili ya kujadili utekelezaji wa mkataba wa kwanza wa makubaliano (MOU). Ndomba amesema kuwa, Mkataba wa kwanza wa makubaliano ulisainiwa Novemba 13, 2020 na umekuwa na mchango mkubwa katika kuimarisha mahusiano kati ya taasisi hizi mbili katika kuimarisha…

Read More

Na John Walter-Manyara. Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga, amemuagiza Katibu tawala Mkoa kuzipitia Halmashauri zote za mkoa wa huo zenye hati zenye mashaka zilizoorodhedhwa na CAG, kufanyiwa Ukaguzi maalum pamoja na kupitia Mikataba yote upya. Ametoa agizo hilo leo Juni 14,2023 katika kikao maalum Cha baraza la Madiwani lililolenga kupitia na kujadili hoja 35 za Mdhibiti na Mkaguzi  Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) zilizotajwa katika Halmashauri ya Mji wa Babati yenye hati ya Mashaka. “Ukaguzi wa maana hapa halmashauri ya mji wa Babati ni muhimu kwa sababu mikataba mingi ina utata” alisisitiza Sendiga Mdhibiti na Mkaguzi  Mkuu…

Read More

Na Geofrey Stephen ,Lushoto Tanga Watu Zaidi ya 5,621 wa Vijiji viwili vya Kizanda na Mayo vilivyoko katika Halmashauri ya Bumbuli Wilayani Lushoto Mkoani Tanga huenda wakaondokana na adha ya kusaka Maji umbali mrefu baada ya Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini(RUWASA) kukamilisha mradi wa Maji wenye thamani ya shilingi milioni 430.9 Hayo yalisemwa na Meneja wa RUWASA Mkoa wa Tanga, Mhandisi Pendo Lugongo mbele ya kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Abdallah Shaibu Kaimu muda mfupi kabla ya kuuzindua mradi huo. Lugongo alisema mradi wa Maji katika Vijiji vya Kizanda na Mayo ni miongoni mwa…

Read More