Author: Geofrey Stephen

Na Mwandishi wa Wetu KITETO. WAKULIMA katika Kitongoji cha Napulukunya Kijiji cha Kimana wilayani Kiteto Mkoani Manyara wameiomba serikali kupitia waziri wa Ardhi , Deogratius Ndejembi kuingilia kati mgogoro wa muda mrefu unaofukuta kati yao na wafugaji kufuatia viashirio vya uvunjifu wa Amani vinavyoanza kujitokeza. Aidha wakulima hao zaidi ya 70 wanamtuhumu mkuu wa wilaya hiyo,Remidius Mwema pamoja na Mbunge wa jimbo la kiteto,Edward Lekaita kuchochea mgogoro huo kwa kupendelea wafugaji ambao wamekuwa wakiingiza mifugo yao kwenye mashamba yao na kufanya uharibifu wa mazao bila kuchukuliwa hatua stahiki. Wakiongea na vyombo vya habari kwa niaba ya wenzao ,Singilbert Silayo,Deogratiaus Kulaya…

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha . MAKAMUwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ametoa rai kwa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) kukamilisha mchakato wa kusanifu na kujenga Mfumo Mkuu wa Ubadilishanaji Taarifa Serikalini na kuhakikisha Taasisi zote za umma zinajumuishwa katika mfumo huo. Makamu wa Rais ametoa rai hiyo wakati wa Ufunguzi wa Kikao Kazi cha Tano cha Mamlaka ya Serikali Mtandao kinachofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC). Amesema Jambo hilo ni muhimu ili kurahisisha utendaji kazi katika taasisi na kurahisisha utoaji huduma kwa wananchi kama ilivyoelekezwa na Rais wa Jamhuri ya…

Read More

Na Bahati Siha, Kaimu Mkurungenzi mkuu wakala wa maji safi na usafi wa mazingira (RUWASA)Wolta Kirita, amesema Ruwasa imeingia kwenye makubaliano na chuo cha ufundi kilichopo mkoani Arusha kubuni mitaa kabla ya malipo(prepaid Weter) Ambapo lengo kufunga mita hizo ili kuondoa malalamiko ya Wananchi ya madai ya kubambikiwa bili , kukabiliana na changamoto ya malimbikizo ya madeni na kuongeza ufanisi wa ukusanyaji mapato ya Serikali. Haya yamesemwa February 8 ,2025 na Kaimu Mkungenzi huyo katika ziara ya kutembea Bodi ya maji ya Lawate fuka iliyopo Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro kwa lengo la kuangalia skimu inavyofanya kazi,ambapo pia ameambatana na wajumbe…

Read More

Na Geofrey Stephen Monduli Arusha Mapema leo Familia ya Eduard Ngoyai Lowassa ikiongozwa na Mama Regina Lowassa wafanya Misa ya shukurani katika Kanisa la Kiinjili Kilutheri la Tanzania Dayosisi ya Kaskazini KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati Jimbo la Maasai Kati, Usharika wa Monduli. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene ameungana na wanafamilia, viongozi wa chama,Serikali na wananchi katika ibada ya Shukrani ya Hayati Edward Ngoyai Lowassa Waziri Mkuu Mstaafu iliyofanyika katika Kanisa la KKKT Monduli Mjini Mkoani Arusha, AIDHA WAZIRI SIMBACHAWENE ASHIRIKI IBADA YA SHUKRANI YA HAYATI WAZIRI MKUU…

Read More

Na Mosses Mashala Zanzibar. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amewahimiza Wafanyabiashara kujiandaa na Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kufanya Biashara kwa Uadilifu na kuwa na Huruma kwa Wananchi. Alhaj Dkt.Mwinyi ameyasema hayo alipozungumza na Waumini wa Dini ya Kiislamu wa Masjid Jibril Mkunazini alipojumuika katika Sala ya Ijumaa. Aidha Alhaj Dkt.Mwinyi amesema kumekuwa na kawaida na tabia ya Baadhi ya Wafanyabiashara kupandisha bei Bidhaa wakati huo. Amefahamisha Kuwa Serikali imekuwa ikipunguza Ushuru katika Mwezi wa Ramadhani hivyo si jambo jema kwao kupandisha bei za bidhaa na kuwaongezea mzigo Wananchi . Akizungumzia suala la…

Read More