Author: Geofrey Stephen

Na Geofrey Stephen ,Monduli Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Professa Aldof Mkenda amesema kuwa serikali inajali ulinzi na usalama wa mtoto wa kike sehemu ya kazi na ndio maana inasisitiza muhimu wa elimu kwa jinsi hiyo. Waziri Mkenda ameyasema hayo Wilayani Monduli Mkoani Arusha katika  Chuo Cha Maendeleo-Mto wa Mbu{FDC} wakati akizindua mwongozo na Mafunzo ya Ulinzi na Usalama wa Mwanamke na Vijana katika kupiga vita unyanyasaji kijinsia na kingono. Alisema serikali inajali na kutamnua  ulinzi na usalama wa mtoto wa kike na kiume katika mafunzo ya taasisi mbalimbali Nchini ya ufundi stadi na ndio maana inaingia gharama kubwa kutafuta wataalamu…

Read More

 Na Pendo Mkonyi, Arusha. Shule ya sekondari  Mwandeti ya mkoani arusha imeendelea kuwa kinara  kutokana na matokeo yake mazuri kufuatia mwaka huu  wa 2023 tena  katika matokeo ya kidato Cha 6 kufaulisha Kwa daraja la kwanza watahiniwa wote 77. Akizungumza  mara baada ya kutangazwa Kwa matokeo ya kidato Cha 6 nchini mkuu wa shule ya sekondari Mwandeti John Silvano Masawe amesema kuwa wanafunzi wote 77 waliofanya mitihani Yao ya kidato Cha 6 wamefaulu Kwa kiwango Cha juu na hawezi kulinganishwa na shule ya sekondari Ilboru na kisimiri Pichani: ni mkuu wa shule ya sekondari Mwandeti John Silvano Masawe. Masawe amesema…

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha . Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Nape Nnauye amezindua programu ya Shahada ya Media Anuwai na Mawasiliano kwa Umma katika chuo cha uhasibu Arusha-Kampasi ya Arusha . Akizindua kozi hiyo Nape amesema kuwa,kitendo cha kuzinduliwa kwa programu mpya chuoni hapo ni jambo kubwa sana  kwa maslahi ya nchi na linapaswa  kuigwa  na vyuo vingine ili kuweza kupata wataalamu wengi zaidi waliobobea katika fani hiyo. Nape amesema kuwa,kuwepo kwa programu hiyo katika chuo hicho kutasaidia kupata wataalamu bora na wa kipekee  waliobobea na kuondokana na changamoto  ya kuwa na wanataaluma  katika fani  hiyo ambao hawajabobea …

Read More

Na Doreen Aloyce, Dodoma Serikali ya Kanada imetoa kiasi cha Shilingi Bilioni 240 kwenye Mfuko wa Afya ya pamoja (Health Basket Fund) ili kusaidia Sekta ya Afya nchini. Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amebainisha hayo leo Julai 20, wakati wa mkutano wa utekelezaji wa shughuli za Mfuko wa Afya wa Pamoja (Health Busket Fund) HBF na Waziri wa Maendeleo ya jamii Kanada Jijini Dodoma. “Tunaishuku sana Serikali ya Kanada kupitia Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Kanada Mhe. Harjit Sajjan kwa kusaidia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kiasi cha shilingi Bilioni 240 kwa ajili ya kuboresha sekta…

Read More

Magonjwa yasiyoambukiza huchangia asilimia 33 ya vifo nchini. Na. Catherine Sungura, Dodoma Magonjwa Yasiyoambukiza (NCDs) yanachangia takribani 33% ya vifo vyote nchini huku kwa takwimu za Shirika la Afya duniani (WHO) kwa mwaka 2020 zinaonesha kuwa magonjwa hayo yalichangia zaidi ya vifo milioni 41 sawa na 71% ya vifo vyote Duniani ukilinganisha na vifo milioni 57 kwa mwaka 2016 duniani. Hayo yameelezwa leo na Waziri wa Afya kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Ally Mazrui wakati wa Uzinduzi wa Utafiti wa Kitaifa wa Viashiria vya Magonjwa Yasiyoambukiza (STEPS SURVEY 2023) uliofanyika kwenye ukumbi wa Tawimu Jijini Dodoma. Mhe. Mazrui amesema…

Read More