Author: Geofrey Stephen

BRYSON MSHANA, TABORA Mashindano ya umoja wa Michezo na taaluma kwa wanafunzi wa Shule za Mshingi Tanzania (UMITASHUMTA) yamefunguliwa Mjini Tabora ambapo yanafanyika kitaifa na kuhusisha mikoa yote ya Tanzania. Mashindano hayo amabayo yanahusisha michezo mbalimbali yamefunguliwa Juni 03, 2023 na Naibu Katibu mkuu anayeshughulikia Elimu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), Dr. Charles Msonde. Katika hotuba yake Dr. Charles Msonde amesisitiza juu uadilifu wakati wa michezo ya UMITASHUMTA mwaka huu wa 2023, ikiwepo udhibiti wa wanamichezo wasioruhusiwa (MAMLUKI) ili kuipa heshima sekta ya michezo mashuleni. Msonde amesisitiza juu kuzingatia miongozo iliyowekwa kwa…

Read More

Na Doreen Aloyce,Dodoma Kufuatia kifo cha aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) Marehemu Nusura Hassan ABdallah Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imetoa matokeo ya uchunguzi wa Kifo chake na kidai kwamba kilitokana na Kisukari Taarifa hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Tume hiyo ,Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu wakati alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari Jijini Dodoma na kusema kuwa kazi ya uchunguzi wa kifo hicho umekamilika kwa mujibu wa Kifungu cha 15(1)(a) cha Sheria ya THBUB, Sura ya 391, kinachoipa uwezo wa kuanzisha uchunguzi. Ambapo katika uchunguzi huo Jaji Mstaafu Mwaimu amebainisha maeneo yoye yaliyohisishwa…

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale ,serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Simai Mohammed Said amesema ni lazima utamaduni wa asili ikiwemo maajabu ya miti mbalimbali utangazwe ili kuvutia watalii wengi kufika nchini. Aidha alisisitiza ushirikiano uliopo baina ya nchi ya Tanzania na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ili kutangaza zaidi vivutio vya utalii vilivyopo katika nchi hizo mbili. Hayo ameyasema wakati akifungua Maonyesho ya Utalii ya Karibu -Kill Fair 2023 yanayofanyika kwa siku ya tatu eneo la Viwanja vya Magereza Jijini Arusha. Alisema nchi ya Tanzania imefungua fursa za utalii kutokana na fursa iliyotangazwa kupitia filamu ya…

Read More

Na Ahmed Mahmoud Imeelezwa kwamba Suala la elimu  Vipimo ni kiungo muhimu katika mnyororo mzima wa thamani na zana muhimu ya kuthibitisha ubora wa bidhaa hivyo elimu hii iende hadi vijijini Ili kusaidia makundi kuokoa jamii yetu. Akifungua Maadhimisho ya siku ya Vipimo Duniani na hapa nchini Kwa Kanda ya kaskazini Jijini Arusha Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhandisi Emmanuela Kaganda Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha amesema kwamba Ili usalama wa chakula Vipimo ni muhimu Sana Kwa watumiaji katika kuondoa changamoto ya utunzaji wa vyakula huko vijijini . Ametoa Rai Kwa washiriki wa Maadhimisho hayo na Watanzania…

Read More

Na Geofrey Stephen  Arusha  Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limemfikisha mahakamani mtuhumiwa Isaack Mnyangi (45)Mkazi wa Sombetini Jijini Arusha na kusomewa shtaka moja la shambulio la Kudhulu Mwili. Mbele ya Hakimu ,Jenifa Edward wa mahakama ya wilaya Arusha,katika kesi namba 80 ya mwaka 2023,mwendesha mashtaka wa serikali ,Charles Kagilwa akisaidiana na Godfrey Nungu na Callorine Kasubi,alidai  mnamo Mei 23 mwaka huu majira ya saa tano usiku katika eneo la Osunyai kwa Diwani jijini Arusha   Mshtakiwa Mnyangi alimshambulia Jackline Mkonyi(38)ambaye ni mke wake na kumng’oa jino moja ,kumpiga kwa Mkanda Usoni na mgongoni na maeneo mengine ya mwili wake…

Read More

Na Doreen Aloyce, Dodoma Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamepatiwa mafunzo kuhusu majukumu na fursa zilizopo katika ofisi ya Hakimiliki Nchini CoSOTA ikiwemo kulinda hakimiliki za Wabunifu hapa nchini. Wakipatiwa semina hiyo katika ukumbi wa Msekwa bungeni jijini Dodoma na kufunguliwa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana ambapo amesema lengo ni kueleza fursa za kibiashara zilizopo katika Hakimiliki pamoja na kuongeza uelewa kuhusu taasisi hiyo. “Sekta ya Ubunifu nchini inakua siku hadi siku, sisi upande wa Serikali tunandelea kuhakikisha Wabunifu wananufaika na kazi zao pamoja na kuwaelemisha kuhusu umuhimu…

Read More