Na *Mwl.Mohamed Mwampogwa* -LUSHOTO TANGA_ ____________________________________ _Yapo baadhi ya mambo huonekana niya kawaida unapo yasikia au kuyaona yametendeka mahala fulani lakini katika uhalisia kwa wahusika waliofanya matukio hayo na Jamii yao hubaki kama jambo lenye maajabu na kugusa Historia ya maisha yao._ _Hili limetokea katika Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 Wilayani Lushoto kwa kuweka historia kwani Baba Askofu mkuu Dr.Mbilu wa kkkt dayosisi ya kazkazini Mashariki ashiriki mbio za Mwenge wa Uhuru 2023._ _”Haikuwahi kutokea kuona Kiongozi kama huyu Dk.Mbilu kuweza kushiriki kukimbiza Mwenge,iliamsha hisia za Upendo,mwenyewe nilihisi Roho wa Mungu wetu yupo pamoja nasi,tunawashukuru Viongozi wetu wa Chama…
Author: Geofrey Stephen
Na Mwandishi wa A24Tv lushoto Tanga . _Masista wa Mazinde Juu Wilayani Lushoto Mkoani Tanga wamestaajabu kuushika mwenge wa Uhuru ulipofikishwa katika maeneo yao._ _”Kwakweli haijawahi kutokea heshima kama hii kuushika huu Mwenge wa Uhuru,Mungu ambariki Mkuu wa Wilaya yetu Mhe.Kalisti Lazaro kwa Upendo huu,Mungu ambariki Mama yetu Dk.Samia” alisikika Sista mmoja akisema._ _Mwenge wa Uhuru umemaliza mbio zake leo tarehe 16.06.2023 ambapo umezunguuka katika Halmashauri mbili za Wilaya ya Lushoto na Majimbo matatu hata hivyo miradi yote imepita vyema na kuwekewa mawe ya Msingi._ _Wananchi wa Walaya ya Lushoto wamewapongeza sana Viongozi wa Chama na Serikali,Waheshimiwa Wabunge na Watumishi…
Na Geofrey Stephen , Handeni Miradi 8 yenye gharama ya Zaidi ya shilingi Bilioni 1.2 itazinduliwa na kuwekwa jiwe na Msingi katika Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga na Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa. Hayo yalisemwa na Kaimu Mkuu wa Wilaya hiyo Kalisti Lazaro alipokabidhiwa Mwenge wa Uhuru Kitaifa na Mkuu wa Wilaya Korogwe Joketi Mwenegoha ulipomaliza kukimbiwa katika Halmashauri ya Korogwe Vijijini. Lazaro alisema kuwa Mwenge wa Uhuru Kitaifa ukiwa katika Wilaya ya Handeni utakimbizwa umbali wa km 187.3 katika Kata 8 za Wilaya hiyo ikiwa ni pamoja na kufungua mradi mmoja,miradi miwili itatembelewa na kuonwa na miradi Murano…
Na Richard Mrusha kahama MKURUGENZI wa Manispaa ya Kahama ,Mkoani shinyanga Anderson Msumba amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Kwa kuendelea kumwamini na kumuacha aendelee kuiwakilisha vyema Serikali Kwa kuwatumikia wananchi wa Manispaa hiyo. Amesema anamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan Kwa kumuamini na kuendelea kumuacha kwenye kituo chake cha Kahama ili aiendelee kumuwakilisha kuendelea kuwatumikia wananchi Kwa kutatua kero mbalimbali ndani ya Manispaa hiyo. Msumba ameyasema hayo wilayani humo Juni 14 ofisni kwake katika mahojiano maalumu na waandishi wa Habari juu ya maendeleo ya Manispaa hiyo ambapo Amesema kuwa ataendelea kufanya kazi Kwa weredi ili kuweza kusonga mbele katika kuwaletea…
Leo June 17, 2023,karibuArusha24tv kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za nyuma za Magazeti ya Tanzania . Hii ni A24tv Mwisho .
Mwenge wa Uhuru kitaifa na matukio mbali mbali Wilayani Lushoto Mkoani Tanga ulivyo zunguka na kuzindua miradi mbali mbali na wananchi kupata Fursa ya kupiga nalo picha sio wakubwa tu na mpaka watoto wadogo wabeba mwenge wa uhuru Mtoto ambaye ajafahamika Majina yake akiwa katika kati ya watumishi wa halmashauri ya Lushoto wakati wa kupokea Mwenge wa Uhuru kitaifa wilayani lushoto akiwa amebeba mwenge wa uhuru Masista wa St Mary’s Mazinde Juu secondary Lushoto, shule bora kitaifa ya wasichana Lushoto Wakipokea mwenge wa uhuru
Na Geofrey Stephen Lushoto Tanga Matukio katika picha likionyesha uzinduzi wa daraja la kisasa la mlesa kata ya Dule M wilayani lushoto ambapo Mwenge wa Uhuru Kitaifa ulizindua mradi huo mkubwa wa garama ya shilingi Milioni 270,892 ,140.00 fedha zinazotokana na tozo ya mafuta . Mradio huu umeanza kutekelezwa mnamo tarehe 02 mwezi wa 11,2022 ambapo ulitarajiwa kukamilika ambapo kwa sasa mradi upo kwenye kipindi mtazamio . Aidha katika utekelezaji wa mradi huo makundi mbali mbali ya wananchi walipata fursa ya kunufaika kwa kupata ajira za muda pia mradi baada ya kukamilika umefanikisha kuondoa adha ya usafirishaji iliyo dumu kwa…
Na Doreen Aloyce, Dodoma Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene, ameipongeza Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) kwa jitihada kubwa inazozifanya katika kukuza na kuimarisha Serikali Mtandao nchini. Simbachawene ameitoa pongezi hizo jana, alipofanya ziara ya kikazi katika Ofisi za Mamlaka ya Serikali Mtandao zilizopo Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma, kwa lengo la kukagua utekelezaji wa majukumu ya e-GA katika usimamizi wa matumizi ya TEHAMA kwenye taasisi za umma. Amesema kuwa, kuimarika kwa matumizi ya TEHAMA katika taasisi za umma, kunatokana na usimamizi mzuri wa e-GA katika kuimarisha jitihada…
Karibu Arusha A24Tv Kutazama Habari kubwa katika Magazeti ya leo ya Tanzania kilicho Andikwa Mbele na Nyuma Hii ni A24Tv . Mwisho.
Na Geofrey Stephen Lushoto . Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa,Abdalah Shaib Kaim,ametaka mradi wa Zahanati unaojengwa kwa gharama ya sh,mil 100.9 katika kijiji cha Kwemakame,wilayani Lushoto ,Mkoani Tanga, kukamilika kwa wakati ili kusaidia huduma ya Afya kwa wananchi wanaotembea umbali mrefu wa zaidi ya km 25 kufuata huduma hiyo. Akiongea wakati mbio za mwenge wa Uhuru zilipotembelea Zahanati hiyo na kuweka jiwe la msingi,Kaim alimshukuru rais Samia suluhu Hassan kwa kuwezesha mradi huo na kutoa rai kwa wasimamizi wa mradi kuhakikisha unakamilika kwa wakati ili kuwapunguzia wananchi adha ya huduma ya afya . “Serikali imekuwa ikitoa fedha…