Na Doreen Aloyce, Dodoma Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) inalenga kuimarisha zaidi uhusiano wake na Chuo Kikuu cha Mzumbe kupitia mkataba wa makubaliano (MOU) unaotarajiwa kufanyiwa maboresho hivi karibuni. Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa e-GA Eng. Benedict Ndomba, wakati wa kikao cha Pamoja kati ya e-GA na Chuo Kikuu cha Mzumbe kilichofanyika leo katika ofisi za e-GA jijini Dodoma, kwa ajili ya kujadili utekelezaji wa mkataba wa kwanza wa makubaliano (MOU). Ndomba amesema kuwa, Mkataba wa kwanza wa makubaliano ulisainiwa Novemba 13, 2020 na umekuwa na mchango mkubwa katika kuimarisha mahusiano kati ya taasisi hizi mbili katika kuimarisha…
Author: Geofrey Stephen
Na John Walter-Manyara. Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga, amemuagiza Katibu tawala Mkoa kuzipitia Halmashauri zote za mkoa wa huo zenye hati zenye mashaka zilizoorodhedhwa na CAG, kufanyiwa Ukaguzi maalum pamoja na kupitia Mikataba yote upya. Ametoa agizo hilo leo Juni 14,2023 katika kikao maalum Cha baraza la Madiwani lililolenga kupitia na kujadili hoja 35 za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) zilizotajwa katika Halmashauri ya Mji wa Babati yenye hati ya Mashaka. “Ukaguzi wa maana hapa halmashauri ya mji wa Babati ni muhimu kwa sababu mikataba mingi ina utata” alisisitiza Sendiga Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu…
Na Geofrey Stephen ,Lushoto Tanga Watu Zaidi ya 5,621 wa Vijiji viwili vya Kizanda na Mayo vilivyoko katika Halmashauri ya Bumbuli Wilayani Lushoto Mkoani Tanga huenda wakaondokana na adha ya kusaka Maji umbali mrefu baada ya Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini(RUWASA) kukamilisha mradi wa Maji wenye thamani ya shilingi milioni 430.9 Hayo yalisemwa na Meneja wa RUWASA Mkoa wa Tanga, Mhandisi Pendo Lugongo mbele ya kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Abdallah Shaibu Kaimu muda mfupi kabla ya kuuzindua mradi huo. Lugongo alisema mradi wa Maji katika Vijiji vya Kizanda na Mayo ni miongoni mwa…
Karibu Arusha24Tv leo Juni 14, 2023,tunakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za nyuma za Magazeti ya Tanzania Hii ni A24Tv . Mwisho
Na Doreen Aloyce, Dodoma. Meneja Mawasiliano Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), Bi. Subira Kaswaga, amezitaka Taasisi za Umma nchini kuendesha vikao kidijitali kwa kutumia mfumo wa e-Mikutano ili kupunguza gharama za uendeshaji wa vikao. Kaswaga ametoa rai , alipofanya mazungumzo na mwandishi wetu ofisini kwake jijini Dodoma kuhusu faida zitokanazo na mfumo wa e-Mikutano. Amebainisha kuwa, mfumo wa e-Mikutano unawawezesha watumishi wa Taasisi za umma kufanya vikao kidijitali mahali walipo bila kulazimika kukutana mahali pamoja na hivyo kusaidia kupunguza gharama za uandaaji na uendeshaji wa vikao. “Mfumo huu wa e-Mikutano unazisaidia taasisi za umma kupunguza gharama za uendeshaji wa vikao,…
Juni 13 Karibu Arusha24Tv kutazama habari kubwa katika Magazeti ya leo ya Tanzania mbele na nyuma Hii ni A24Tv . Mwisho
Na Geofrey Stephen Lushoto Miradi 17 yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 2 inatarajiwa kuzinduliwa na Mbio za Mwenge Kitaifa katika wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga na Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kuwasili katika wilaya hiyo kesho na utazunguka katika Wilaya hiyo kwa umbali wa km 304. Akizungumza na Waandishi wa Habari Leo ofisini kwake,Mkuu wa Wilaya ya Lushoto,Kalisti Lazaro alisema kuwa Mwenge utapokelewa Lushoto katika Kijiji Cha Samata kilichopo Halmashauri ya Bumbuli na utazungushwa katika Halmashauri hiyo kwa umbali wa km 122 na miradi 9 itazinduliwa yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni 779. Kalisti Lazaro akizungumza na Vyombo…
Na Geofrey Stephen Arusha Watetezi wa Haki za Binadamu nchini Tanzania wameiomba serikali kusitisha zoezi la kubadili vijiji 14 na kuwa pori tengefu la Pallolet ili kulinda, kuhifadhi na kuendeleza haki za binadamu kwa wananchi wa Tarafa ya Loliondo na sehemu ya Tarafa ya Sale. Ombi hili la watetezi wa haki za binadamu limekuja baada ya watetezi hao kufanya ziara mwezi Mei katika vijiji vya Msomera wilayani Handeni mkoani Tanga, Tarafa ya Loliondo na Sale wilayani Ngorongoro mkoani Arusha ili kuangalia hali ya haki za binadamu katika maeneo hayo. Odero Charles Odero, Mkurugenzi CILAO akizungumza na waandishi wa habari ofisini…
Karibu Arusha24Tv leo Juni 12 Kutazama kilicho Andikwa Katika Magazeti ya leo ya Tanzania Mbele na Nyuma Hii ni A24Tv . Mwisho .
Juma pili ya leo Juni 11, 2023,Tunakukaribisha Arusha24Tv kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za nyuma za Magazeti ya Tanzania. Hii ni A24Tv. Mwisho.