Author: Geofrey Stephen

Na Pamela Mollel,Arusha Jamii imeaswa kuzingatia maadili na kuacha vitendo viovu na kufanya yale yanayo mpendeza Mungu ikiwemo kufanya kazi kwa bidii na uaminifu katika nafasi tunazopewa ili nchi iweze kuwa na maendeleo na kupiga hatua kiuchumi. Hayo yameelezwa na Baba Askofu Dkt. Solomoni Jacob Massangwa ambae pia ni Mkuu wa Dayosisi ya kaskazini kati kanisa la kilutheri Tanzania katika ibada ya kumstaafisha parishworker wa jimbo la Arusha Mashariki Bi. Rebeca Christopher Mungure ambae amekuwa kwenye utumishi takribani miaka 40. Askofu Dkt. Solomoni Masangwa alisema kuwa jamii kwa ujumla inapaswa kuiga mfano mzuri kutoka kwa Parishworker huyo aliyejitoa kumtumikia Mungu…

Read More

Na Mwandishi wetu Arusha Mzee Edward Mollel{65} Mkazi wa Sanawari Jijini Arusha ameliomba jeshi la Polisi Mkoani Arusha kufanya kila linalowezekana kumkabidhi maiti ya mwanaye,Faraja Mollel{8} aliyechinjwa kinyama na watu watatu wanaojulikana ambao walitumwa na Mfanyabiashara Maarufu ya Madini ya Tanzanite Jijini Arusha kwa manufaa yake vinginevyo atamwona Rais Dk Samia Suluhu Hassan ili aweze kumsaidie. Mollel alisema waliofanya tukio hilo wote wamekamatwa na Polisi Arusha ni pamoja na Amina Poul maarufu kwa jina la Ester ambaye ni mpangaji wake  katika nyumba anazomiliki eneo la nyumbani kwake Sanawari ,Mganga wa kienyeji mkazi wa Babati aliyemtaja kwa jina la John Mtai…

Read More

Na Doreen Aloyce ,Dodoma KATIBU MKUU Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi amepongeza maendeleo ya ujenzi wa Uwanja wa Mashujaa unaojengwa katika Mji wa Serikali, Mtumba Jijini Dodoma. Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi (kulia) akiwa na Mratibu wa Kamati ya zoezi la Serikali kuhamia Dodoma Bw. Meshack Bandawe wakikagua Eneo la mradi wa Ujenzi wa Mnara wa Mashujaa Mtumba Dodoma. Dkt. Yonazi ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kutembelea na kukagua ujenzi huo ambapo ameeleza kwamba unaendelea vizuri na unatarajiwa kukamilika mapema kabla…

Read More

John Walter -Arusha. Benki ya NCBA imetoa msaada wa vifaa tiba katika kituo cha Afya cha Kitumbeine kilichopo Wilayani Longido Mkoani Arusha kwa lengo la kuwasaidia wakinamama wajawazito wasioweza kujifungua kwa njia ya kawaida kufanyiwa upasuaji ili kuokoa Maisha ya Mama na Mtoto ambao walikua wakitembea umbali mrefu kufuata huduma za upasuaji katika hospitali ya Wilaya. Akikabidhi Msaada huo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NCBA Claver  Serumaga amesema kuwa benki hiyo imejizatiti katika kusaidia jamii inayowazunguka  na katika kipindi wameamua  kutoa msaada huo katika katika kituo cha Afya cha Kitumbeine kinachohudumia Zaidi ya watu 40,000. Mkurugenzi huyo amesema kuwa wametoa…

Read More

Na Mwandishi wa A24Tv ,Mirerani Rufaa ya kupinga maamuzi ya Kamati juu ya mgogoro wa uchimbaji kati ya mgodi wa Kampuni ya Gem & Rock Venture uliopo kitalu B na kampuni ya Franone inayomiliki mgodi wa kitalu C na serikali iliyopo Mirerani  iliyokatwa na Gem & Rock Venture kwa Katibu Mkuu Wizara ya Madini Kheri Mahimbali imetupiliwa mbali ya kampuni hiyo imeamuriwa kufuata maamuzi na masharti ya kamati yaliyotolewa march 28 mwaka huu na sio vinginevyo. Katibu Mkuu Wizara ya Madini Kheri Mahimbali. Kwa mujibu wa taarifa ya awali ya Afisa Mfawidhi wa Madini Mirerani ,Mernad Msengi ilisema kuwa Machi…

Read More

Na John Walter-Manyara Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura) imewataka wanafunzi wanaohitimu vyuo vya ufundi katika fani ya umeme kuwa na leseni inayowatambua kulingana na viwango vyao. Hayo yamesemwa leo Juni 5, 2023 na Meneja wa Ewura Kanda ya Kaskazini, Mhandisi Lorivii Long’idu wakati akizungumza na wanafunzi wa masomo ya umeme katika Chuo cha Ufundi Veta Manyara kilichopo mjini Babati, wakati wa utoaji elimu maalum kwa wanafunzi hao juu ya umuhimu wa kuwa na leseni. Amesema leseni hizo zina madaraja tofauti na zinatolewa kwa kuzingatia ujuzi, elimu na uzoefu katika kufunga umeme wenye msongo husika. Mhandisi huyo amesema…

Read More