Author: Geofrey Stephen

Na Ahmed Mahmoud Imeelezwa kwamba Suala la elimu  Vipimo ni kiungo muhimu katika mnyororo mzima wa thamani na zana muhimu ya kuthibitisha ubora wa bidhaa hivyo elimu hii iende hadi vijijini Ili kusaidia makundi kuokoa jamii yetu. Akifungua Maadhimisho ya siku ya Vipimo Duniani na hapa nchini Kwa Kanda ya kaskazini Jijini Arusha Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhandisi Emmanuela Kaganda Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha amesema kwamba Ili usalama wa chakula Vipimo ni muhimu Sana Kwa watumiaji katika kuondoa changamoto ya utunzaji wa vyakula huko vijijini . Ametoa Rai Kwa washiriki wa Maadhimisho hayo na Watanzania…

Read More

Na Geofrey Stephen  Arusha  Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limemfikisha mahakamani mtuhumiwa Isaack Mnyangi (45)Mkazi wa Sombetini Jijini Arusha na kusomewa shtaka moja la shambulio la Kudhulu Mwili. Mbele ya Hakimu ,Jenifa Edward wa mahakama ya wilaya Arusha,katika kesi namba 80 ya mwaka 2023,mwendesha mashtaka wa serikali ,Charles Kagilwa akisaidiana na Godfrey Nungu na Callorine Kasubi,alidai  mnamo Mei 23 mwaka huu majira ya saa tano usiku katika eneo la Osunyai kwa Diwani jijini Arusha   Mshtakiwa Mnyangi alimshambulia Jackline Mkonyi(38)ambaye ni mke wake na kumng’oa jino moja ,kumpiga kwa Mkanda Usoni na mgongoni na maeneo mengine ya mwili wake…

Read More

Na Doreen Aloyce, Dodoma Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamepatiwa mafunzo kuhusu majukumu na fursa zilizopo katika ofisi ya Hakimiliki Nchini CoSOTA ikiwemo kulinda hakimiliki za Wabunifu hapa nchini. Wakipatiwa semina hiyo katika ukumbi wa Msekwa bungeni jijini Dodoma na kufunguliwa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana ambapo amesema lengo ni kueleza fursa za kibiashara zilizopo katika Hakimiliki pamoja na kuongeza uelewa kuhusu taasisi hiyo. “Sekta ya Ubunifu nchini inakua siku hadi siku, sisi upande wa Serikali tunandelea kuhakikisha Wabunifu wananufaika na kazi zao pamoja na kuwaelemisha kuhusu umuhimu…

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha Jumla ya walim 500 wa shule za sekondari nchini wameanza kupatiwa mafunzo ya matumizi sahihi ya Tehama na Vishkwambi ili kupata mbinu mpya ya kuzitumia kwenye kufundishia. Mafunzo hayo yamekuja ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Rais Samia Suluhu aliyoyatoa siku ya Mei mosi 2023 baada ya kusoma moja ya bango la walimu walioomba kupatiwa mafunzo ya jinsi ya kutumia vishkwambi kufundishia. Akifungua mafunzo hayo mkoani Arusha, Naibu katibu mkuu wizara yenye dhamana ya Elim, Dkt. Franklin Rwezimula alisema mafunzo hayo ya siku tano yanalenga kuwafundisha walimu 1500 walioko kazini mbinu mpya za matumizi ya Tehama…

Read More

Mwandishi wetu, Longido maipacarusha20@gmail.com Longido.Shirika la wanahabari wanaosaidia Jamii za pembezoni (MAIPAC) limebaini uwepo wa matukio ya ukeketaji kwa watoto waliochini ya miaka mitano wilayani Longido mkoa wa Arusha. Baadhi ya wazazi wa Jamii ya kifugaji katika Wilaya hiyo,wameanza kuwakeketa watoto wakiwa wachanga ili kukwepa kukamatwa na vyombo vya dola. Wakizungumza na timu ya waandishi wa habari wanachama wa MAIPAC wanaofanya uchunguzi juu ya kuibuka matukio ya ukeketaji watoto ,Wilaya ya Longido mkoa wa Arusha,baadhi ya wazazi na maafisa wa serikali wilaya ya Longido walisema…

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha. Kadinali wa pili wa kanisa la Ngurumo ya upako linaloongozwa  na Nabii Mkuu Mh Dkt Geordavie jijini Arusha, Elizaberth Humphrey amemshukuru MUNGU kwa jambo kubwa lililofanyika tarehe 28 Mwezi May 2023  katika kanisa hilo kwa kumpa tuzo Nabii mkuu Dkt GeorDavie. Amesema tangu walipofika Ngurumo ya Upako kwa Nabii Mkuu GeorDavie mahali amefanyika kuwa baraka Kubwa sana kwao kwasababubu amekuwa mtu mwenye matendo yenye kugusa mioyo ya watu wengi. Amesema kuwa amekuwa Baba Mwema kwa watu wote bila kujali kabila wala Dini ndio maana watoto wake mbele za MUNGU kwetu sisi wote. Amesema alitutoa kwenye matatizo…

Read More