Author: Geofrey Stephen

Kuhusu siku yake ya kuzaliwa Nabii Mkuu Mh  GeorDavie kwanini kuna kuwa na kumbikizi ?  Na Geofrey Stephen Arusha . Tarehe 25 Mwezi April ni kumbukizi ya Nabii Mkuu Mh Dokta  GeorDavie kukumbuka siku yake ya kuzaliwa ambapo Maelfu ya  waumini wa huduma ya Ngurumo ya Upako walisherekea kwa pamoja huku wageni kutoka nchi mbali mbali   kutoka nchini  Congo, South Africa, Kenya na maeneo mbali mbali ya pembezoni  ya dunia  walikuwepo katika siku hii muhimu kwa Nabii Mkuu. Awali akizungumzia siku hiyo muhimu kwake Mh Nabii Geordavie Mkuu amesema kwamba siku hiyo ilikuwa ifanyike tarehe 25 mwezi April lakini kutokana…

Read More

Na Doreen Aloyce, Dodoma SERIKALI imesema kuwa Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) inatumika kama Nyenzo kwa serikali ili kuhakikisha yale mapungufu yote yaliyobainika yanafanyiwa kazi kwa maslahi mapana ya Taifa. Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari -MAELEZO Gerson Msigwa amesema kufuatia Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) mapungufu yote yatafanyiwa kazi ili kukomesha vitendo vya ubadhilifu wa Fedha. Pia ripoti hiyo inatumika kama Nyenzo kwa serikali ili kuhakikisha yale mapungufu yote yaliyobainika yanafanyiwa kazi kwa maslahi mapana ya Taifa. Hayo ameyabaisha wakati alipokuwa akizungumza na…

Read More

Na Doreen Aloyce,Dodoma Mbunge wa jimbo la Mwanakwerekwe Visiwani Zanzibar Khasimu Hassan Haji ameishukuru serikali kupitia Rais Samia suluhu Hassan na Dkt Hussein Ally Mwinyi kwa jinsi walivyoleta miradi ya maendeleo ya miundo mbinu jimboni kwake jambo ambalo limesaidia kuinua uchumi wa Zanzibar. Kauli hiyo ameitoa Bungeni Dodoma wakati alipokuwa akizungumza na Vyombo vya habari juu ya maendeleo yaliyopo jimboni kwake kutokana na uchapakazi wa Serikali tofauti na hapo awali . Amesema kuwa kupitia fedha ya Uviko 19 iliyoletwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassani imeweza kujenga shule ya msingi ya ghorofa moja , mradi…

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha VIONGOZI mbalimbali wa dini, Chama na serikali Mkoa wa Arusha, wamemwagia sifa FANYABIASHARA Maarufu wa Madini jijini Arusha,Faisal Shahbhai wakidai ni mfano wa kuigwa ,mwenye moyo wa kizalendo kutokana na jitihada zake za kupigania maendeleo ya mkoa pamoja na kuwaunganisha wafanyabiashara wadogo na serikali yao . Akiongea katika hafla ya chakula cha jioni kwa ajili ya kufuturisha waislamu ,kilicho andaliwa na mfanyabiashara huyo kwa kushirikiana na chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha ,mkuu wa mkoa huo, John Mongella alidai kuwa Mkoa unajivunia kuwa na wafanyabiashara wazalendo wenye kupenda maendeleo ya Taifa Lao. Mkuu huyo wa…

Read More

Na Geofrey Stepben 24tv Arusha . Katibu Mkuu wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof, Carolyne Nombo ameielekeza ofisi ya mdhibiti ubora wa elimu hapa nchini kuendelea na kufuatilia shule zote za binafsi ili kuweza kubaini shule zinazo fundisha mapenzi ya jinsia moja (ushoga). Prof, Nombo ameyasema hayo leo alipo kuwa akifungua mkutano wa 31 wa Baraza la wafanyakazi wa elimu Jijini Arusha kwa niaba ya Waziri wa elimu,Sayansi na Teknolojia Prof, Adolf Mkenda. Ameeleza kuwa ni vyema kwa Mkurugenzi wa udhibiti ubora kupiga hatua tatu mbele zaidi ili kuweza kukabiliana na changamoto hiyo ambayo hivi sasa inaonekana kukithiri hapa nchini…

Read More